Saturday, March 13, 2010

Oslo Gardemoen

Waombaji ukimbizi 78
warudishwa makwao leo


Hapa watu hao wakisindikizwa na polisi kuingia kwenye ndege kwenye 
uwanja wa Oslo Gardemoen.


Leo kitengo cha polisi kinachoshughulikia wageni; Politiets utlendingsenhet (PU) kimewakamata watu 78 kutoka Serbia na Makedonia walinyimwa haki ya ukimbizi wa kisiasa. Watu hao walikusanywa toka kwenye kambi tofauti za wakimbizi mashariki ya Norway na kupelekwa haraka kwenye uwanja wa ndege wa Oslo Gardemoen.

Norway imeamua kuwa wote wanaokuja kuomba hifadhi za kikimbizi, watajibiwa katika muda wa masaa 48 na kama mwombaji akikataliwa basi anarudishwa alikotoka, na ndivyo walivyofanya safari hii kwa hao waombaji toka Serbia na Makedonia.

Hivi karibuni wameingia watu wengi toka Montenegro, Serbia na Makedonia na kutaka kuomba hifadhi za kisiasa. Hii inatokana na nchi zilizo kwenye makubaliano ya Schengen kufuta viza kwa raia wa nchi hizo kuingia kwenye nchi za Schengen.

Waziri wa sheria, Bw. Knut Storberget alipoulizwa kuhusu hili, alijibu kuwa Norway itachukua wakimbizi wa kweli na sio watu wanaokuja kwa sababu zingine au za kutafuta maisha.

No comments: