Wednesday, March 31, 2010

Oslo, Norway

Wasomali wasio na vibali kurudishwa makwao.
Bw. Terje Sjeggestad, Mkurugenzi Mkuu wa UNE.


Wasomali wote wanaotoka Kusini ya Somalia hadi Mogadishu na ambao wamekataliwa kupewa hifadhi ya kikimbizi, wako kwenye hatari ya kurudishwa Somalia. Uamuzi huo umefikiwa na Halmashauri ya Rufaa ya Uhamiaji, UNE (Utlendingsnemnda), amesema Mkurugenzi Mkuu, Terje Sjeggestad.

Uamuzi huo wa UNE utawagusa karibu Wasomali 3000 waishio Norway bila vibali vya kuishi.

Kwa kipindi kirefu sasa, Wasomali wote ambao wamekataliwa kuishi Norway, wamekuwa wakiishi  bila matatizo kwa sababu hali ya kiusalama haikuwa nzuri ya kuwarudisha. Lakini sasa basi na wataanza kurudishwa.

No comments: