Saturday, April 03, 2010

TEKNOHAMA: leo ni leo asemaye kesho mwongo!


Macworld Video: The iPad Up Close







Wenzetu wanazindua iPad,
sisi tunazindua bia


Hii imenyofolewa toka Tanzanet (The Tanzanian Electronic Networking Community) kwa hisani ya Prof. Mbele

Ndugu

Wikiendi hii kule Tanzania kuna taarifa muhimu ya uzinduzi wa bia mpya. Huku ughaibuni, wikiendi hii watu wako tumbo joto kutokana na kuwa kampuni ya Apple inazindua kifaa kiitwacho iPad, ambacho ni cha kuhifadhia na kusomea vitabu, magazeti, na kadhalika. Ni tekinolojia ya hali ya juu sana katika ulimwengu wa usomaji. 

Kesho ndio siku ya kuzinduliwa iPad, na tayari waMarekani walioagiza wanazidi 250,000. Hii ni pamoja na kuwa bei ya chini kabisa ya kifaa hiki ni yapata dola 500. Kuna aina aina ya kifaa hiki hiki, na aina nyingine bei yake inazidi dola 800. Lakini waMarekani wanapigana vikumbo kukipata.

Kule Ulaya nao wako tumbo joto, hasa kwa vile kampuni ya Apple haijaamua watapelekewa lini au vipi. Tayari kuna wengi wanajaribu kukipata kwa njia zingine, ingawa Apple haijaidhinisha.

Sokomoko la aina hii, eti kwa ajili ya kifaa cha kusomea kitabu, halitokei Bongo. Kule sokomoko ni wakati wa uzinduzi wa bia mpya. Imeripotiwa kwenye blogu ya Michuzi kuwa bia hii mpya imechangamkiwa kwa udi na uvumba na waTanzania.

Watanzania wakiambiwa wanunue kitabu cha shilingi 6000 wanaruka na kulalamikia bei. Lakini uzinduzi wa bia mpya, hata kama kiingilio ni sh. 10,000 watatoa, na humo ndani watazitwanga bia hadi lyamba. Bill ya usiku moja wa haya makamuzi haisemeki.

Sasa Mtanzania, hata kama ni fisadi mwenye vijisenti, hakubali kununua iPad. Isipokuwa anafurahi sana kumsafirisha nanihii Geneva au Jo'burg! kwa shopping ya kufa mtu :-)

Wikiendi hii sitakaa niisahau. 
Wenzetu wanazindua iPad, na sisi tunazindua bia!

-- 
Joseph L. Mbele
English Department
St. Olaf College
Northfield, MN 55057

Phone: (507) 786 3439





Source: http://www.apple.com/



3 comments:

Anonymous said...

Ni kweli usemalo, bongo ni mungu tu anatulinda waja wake.

Huku wameanza kutoa vizuizi kwa wavutaji wa sigara lakini bongo ndo kwanza wamechachamaa ku promote sigara wakati madhara yake wanayaona kabusa vijana wetu wanaangamia.

Zamani akina mama na wasichana walikuwa hawavuti sigara kihivyo lakini leo wamehalalisha na kila mahali.

Wananikera kweli wavuta sigara hawachagui mahali pakuvutia, iwe sehemu ya kilaji au chakula, eti sababu hela yake inaongea kama mwingine anakerwa aanze.

Tutafika kweli?

Mbele said...

Leo ndio uzinduzi wa iPad unaendelea, na foleni zimetanda hapa Marekani. Bofya hapa.

Mbele said...

Leo nimeandika kumbukumbu binafsi kuhusu iPad. Bofya hapa