Saturday, April 03, 2010

Moscow, Urusi

“Mjane mweusi” (Black widow)
huyu anasadikiwa kuwa
alijilipua kwenye metro Moscow

Msichana wa miaka 17, Dzhennet Abdurakhmanova akiwa pamoja na mumewe, Umalat Magomedov. Magomedov aliuawa mwaka 2009 Dagestan, nchi ya shirikisho la Urusi. Picha kutoka AFP/Newsteam/Scanpix.



Mwaka jana Umalat Magomedov mume wa  Dzhennet Abdurakhmanova aliuawa nchini Dagestan iliyo kwenye shirikisho la Urusi. Walikutana na kuoana huku  Dzhennet akiwa na miaka 16. Baada ya mumewe kuuawa, msichana huyo akaamua kulipiza kisasi kama wanavyofanya wanawake wengi walioachwa wajane kwenye nchi za Chechenia, Dagestan, Ingusetia, Ossetia zilizo kwenye shirikisho la Urusi.

Idara ya usalama ya Urusi, Federalnaya Sluzhba Bezopasnosti (FSB) inaamini kuwa; Dzhennet alikuwa mmoja kati ya wanawake wawili waliofanya kitendo cha kigaidi cha kujilipua Jumatatu 29.03.2010 kwenye stesheni ya treni za mjini ya Lubjanka mjini Moscow na kuua watu 39.


No comments: