Hukumu yake yasogezwa mbele kwa
aliyehukumiwa kwa uchawi
Mlebanoni Ali Hussain Sibat, ambaye amehukumiwa kunyongwa kwa kuchinjwa kichwa nchini Saudi Arabia, amepona kwa muda. Wakili wake May el-Khansa ameiambia CNN. Wakili huyo amesema amepewa ahadi hiyo na waziri wa sheria wa Lebanon.
Sibat ni mtabiri na mtoaushauri mwelekezi wa mambo ya kidini kwenye kituo kimoja cha televisheni nchini Lebanon, alikamatwa Medina nchini Saudi Arabia mwaka 2008 alipoeenda kuhiji. Polisi wa maadili wa Saudia walimgundua akiwa miongoni mwa mahujaji, wakamkamata na kumwambia asaini kuwa kweli anafanya mambo ya kiuchawi alikotoka ili wamwachie. Badala yake, waliitumia hiyo karatasi kama amekiri kuwa ni kosa kufanya uchawi au kutabiri kwa sheria za Kiislamu na kumhukumu kifo.
Mpaka sasa haijathibitishwa kama ni kweli, amepona kunyongwa au la.
2 comments:
Sheikh Yahya Hussein,
Usiende Saudi Arabia. Kama ulienda na hukukamatwa, usiende.
Hivi hawa jamaa ina maana hawana hata utabiri wa hali ya hewa?
Manaake kama ni hivyo, basi hata utabiri wa hali ya hewa ni "uchawi"
Iweje huyu Mlebanoni afanye "kosa" Lebanon halafu Saudi Arabia wamhukumu kwao tena jamaa alieenda kuhiji?
Wanasheria nitoeni gizani!
Post a Comment