Sunday, April 04, 2010

Senegal wazindua mnara mkubwa
kuliko ”Statue of Liberty”



Mnara huo ulizinduliwa jana na Rais Abdoulaye Wade, wakiwemo marais kutoka nchi 19, pia alikuwepo mchungaji Jesse Jackson. Mnara huo umejengwa na Wakorea Kaskazini umegharimu Dala za Kimarekani milioni 27. Baadhi ya wanachi wa Senegal wamelaani kuwa mnara huo unakiuka maadili ya Kiislamu na wengine wanadai kuwa unamdhalilisha mwanamke kwa kumwonyesha mwanamme mwenye misuli huku mwanamke akiwa nusu uchi. Wengine wanadai ni ubadhirifu wa hela kwa nchi maskini kama Senegal haswa wakati huu wa tetemeko la uchumi, na wale wanaopinga kwa Rais Wade kutaka kuchukua 35% ya mapato yatakayopatikana kutokana na mnara huo kwa sababu lilikuwa wazo lake. Imam wa msikiti mmoja nchini humo, Massamba Diop ametoa fatwa na kusema kuwa Mungu awanusuru kwa aibu na madhara ya mnara huo.

Watu wengine wanadai kuwa mnara huo ni wa kujivunia kwa Waafrika. Seneta Ahmed Bachir Kounta wa Bunge la nchi hiyo, aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa majengo yote maarufu duniani huwa yanapingwa kwanza kabla ya kukubaliwa: Ametoa mfano wa Mnara wa Eiffel mjini Paris kuwa ulikuwa na upinzani mkubwa kabla ya kujengwa, akatoa mfano wa pili kuwa Statue of Liberty ulipotolewa zawadi kwa Wamarekani kwanza kutoka kwa Wafaransa, ulikataliwa kabla baadaye kukubaliwa.



No comments: