Sir Alex kuachia ngazi msimu wa 2011
Masikitiko kwa wapenzi wa Manchester United: Kocha mkuu wa Manchester United (ManU), Sir Alex Ferguson ameitarifu bodi ya timu hiyo kuwa msimu wa 2011 ndio utakuwa wa mwisho kwake kuifundisha ManU. Sir Alex alianza kuifundisha ManU mwaka 1986 na ameiongoza timu hiyo kwenye zaidi ya mechi 1600 na ni kocha pekee wa timu za England aliyechukua ubingwa mara nyingi ndani na nje.
Inasadikiwa kuwa tayari bodi ya ManU imeanza kutafuta kocha atakayemrithi Sir Alex. Miongoni mwa makocha wanaotabiriwa kuchukua nafasi yake ni: Jose Maurinho wa Inter, Josip Guardiola wa Barcelona, Kocha wa England, Fabio Capello, kocha wa Uturuki, Guus Hiddink, kocha wa Aston Villa, Martin O´Neall na kocha wa Arsenal, Arsene Wenger.
No comments:
Post a Comment