Kwa nini akupasue kichwa?
Mara nyingi watu huwa katika mapenzi wakiwa na lengo la kuja kuwa pamoja. Nakama ilivyo ada ya katabia ka penzi pale mwanzoni kutoka na upya huwafanya mkawa vipofu kutokana na utofauti unajionyesha kati yenu. Tukubali tukatae penzi liliokuwa na maendeleo bora ni lile ambalo wahusika wanaendana kimalengo na mapendeleo. Hata siku moja usiruhusu nafsi yako ikakunyima kuutilia maanani wasiwasi ulikuwa nao juu ya maendeleo ya baadae ya uhusiano wako. Mtihani ni je utajuaje kuwa mambo hayato kuwa mazuri, zifuatazo ni ishara ambazo hutakiwi kuzipuuzia.
HUNARAHA NA UHUSIANO: kuwa katika urafiki ni kitendo sicha kulazimishwa bali ni wewe mwenyewe unataka na hata kutoka ndani ya urafiki huo ni juu yako mwenyewe. Kwa nini ujipasue kichwa wakati umeshona kuna vitu vinavyo kufanya usiwe mwenye raha na kuhisi kama kuna kitu Fulani umekikosa ambacho ulikuwa unakitegemea ukipate kutoka ndani ya urafiki wenu.
HAKUNA JALIANA: ukaribu wenu ni maana tosha ya kujaliana na ndio ambacho hufanya penzi likaonekana hai. Pale itakapoanza kuonekana mmoja kati yenu anajitoa akili na kujiona kuwa anaishi mwenyewe nakufungia vioo uwepo wako basi tambua mwisho wa mkataba wenu umefikia.
MAUZI YA KUKUSUDIA: penzi la ukweli linatawaliwa maelewano na sio kero. Katika hatua nyingine ya kuonyesha dalili za kuvunjika kwa ukaribu wenu mliokuwa nao ni mmoja kufanya vitendo vya makusudi ambavyo vinakera na hata akisisitiziwa kuacha kwake inakuwa kama kupiga gitaa ndani ya chumba cha mashine ya kusagia mahindi. Basi ni bora mkavunja glasi.
KUPOTEA KWA MAWASILIANO: Mawasiliano ni nguzo muhimu sana katika aina hii ya urafiki. Ningumu kuvumilia tabia ya mara kwa mara ya kutokuwa katika nafasi ya kuwasiliana na kama itaanza kutoa hii na kutokuwa na sababu za msingi za kusababisha hilo nadhani ule msemo wa mvumilivu hula mbivu hapa hautakuwa na nafasi.
Jitahidi kutokuwa kipofu ndani ya penzi,kila shetani na mbuyu wake labda huo ulikuwepo si mbuyu wako. (self control is what matters the most)
Imetumwa kwenye blogu hii na mdau anayejiita Tambrina na mtumaji amesema kuwa imenyofolewa toka kwa blogu ya Mbunge mteule Mohammed ”Mo” Dewji.
No comments:
Post a Comment