Monday, November 22, 2010


Mchungaji aliyesema Facebook  haramu;
mzinzi wa ménage à trois

Mchungaji Cedric Miller na mkewe Kim

Mchungaji Cedric Miller aliyewaambia wafuasi wa kanisa lake la the Living Word Christian Fellowship Church, Neptune, New Jersey kuwa kwenye Facebook ni haramu, siri zake zimefichuka (Bofya na soma hii: Mchungaji: facebook ni haramu)

Amegundulika mchezo wake wa kufanya ngono ya watu watatu kwa mpigo (ménage à trois) akiwa yeye, mkewe na mtumishi mmoja wa kiume kwenye kanisa lake! Mchungaji huyo amekuwa akifanya mchezo kila Alhamisi baada ya somo la Biblia na kila Jumapili baada ya misa.

Mchungaji huyo amesema kuwa; mkewe (pichani) amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na msaidizi huyo wa kanisa na mara nyingi amekuwepo wakati mkewe na huyo msaisizi wakifanya mambo yao. Amesema pia wakati mwingine hata mke wa msaidizi huyo wa kanisa alikuwa akishiriki kwenye mchezo huo!


3 comments:

Mtambalike said...

Mnaona jamani, hawa viongozi wa dini zetu, wakati ingebidi wafunge midomo yao kwenye mambo ambayo hayawahusu kama facebook n.k.

Ona sasa huyu ndiye aliyesema kuwa facebook haramu halafu kumbe misa ikiisha anaanza ngono ya mande "ménage à trois...

Hilo alilogusia la Facebook ndio kiangamizi chake.

Mtambalike said...

Nilikuwa nataka kuandika "wakati mwingine ingebidi" nikaishia "wakati ingebidi"

Vidole viliniponyoka!

Anonymous said...

KWELI DUNIA TAMBARA BOVU YAANI WAFALME, MARAIS, MAASKOFU, WACHUNGAJI, MASHEHE, WALALAHAI NA SISI WALALAHOI HAKUNA TOFAUTI!!!!!