Thursday, November 18, 2010

Mchungaji: facebook ni haramu!

Mchungaji, Cedric Miller.

Mmarekani Mchungaji Cedric Miller anasema kuwa mtandao jamii maarufu duniani; Facebook ni haramu kwa sababu unawafanya watu kutamani nje ya ndoa zao. Anadai kuwa mpaka sasa waumini karibu 20 kwenye kanisa lake, wana matatizo ya ndoa kwa sababu ya facebook. Sababu - hao wanandoa 20 wengi wamekutana na wapenzi wao wa zamani kwenye Facebook na hiyo imesababisha matatizo kwenye ndoa zao. Pia ameongeza kuwa si hao tu waliokutana na wapenzi wao wa zamani, wengi wanashindwa kujizuia na majaribu na vishawishi vya kwenye Facebook.

Mchungaji Miller anaongoza kanisa liitwalo  «Living Word Christian Fellowship Church» mjini  New Jersey, lenye waumini 1100.

4 comments:

Mtambalike said...

Kama facebook ni haramu, basi hata kuzunguka kwenye ma´mall (shopping center) ni haramu kwa sababu huko nako tunaona na kukutana na mengi na si huko tu, mengi tu yatakuwa ni haramu. Washkaji huu ni mtazamo wangu..

Anonymous said...

Me too..

Anonymous said...

Yal tell like it is, me too mtazamo wangu..

Anonymous said...

Mchangiaji wa pili na watatu is the same person as mchangiaji wa nne, hamaanishi aliloliandika.