Tuesday, December 14, 2010

Elimu kwa wote:
wanafunzi 584, waalimu 6,
madarasa 2 tu!!!

Baadhi ya madarsa ya shule ya msingi Msiongini Mbuyuni, wilaya ya Uyui, Tabora yakionekana kwa mbele. 

Mmoja wa kati ya waalimu 6 wa shule hiyo.

Na Hastin Liumba,Uyui


MKUU wa wilaya ya Uyui,mkoa wa Tabora,Stanley Kolimba,amestushwa nakushangazwa na taarifa aliyokuwa akisomewa kwenye mkutano wa hadhara,baadaya kusikia kuwa shule ya msingi Mbuyuni,katika kata ya Kigwa,wilayaniUyui,ina wanafunzi 584,walimu 6, vyumba vya madarasa,matundu ya vyoo 6 niviwili tu.

Hayo yalibainika leo, kwenye sherehe za sikukuu ya Uhuru na Jamhuri, zilizofanyika kiwilaya, katika kijiji cha Mbuyuni,kata yaKigwa,wilayani Uyui,mkoani hapa,Akisoma taarifa ya maendeleo ya kata hiyo yenye kijiji kipya,mwalimu mkuu washule ya msingi Mbuyuni,Emanuel Isaya Mwanamiwa,alisema suala la elimukatika shule yake kuna changamoto kubwa kwani shule hiyo ilinzishwa mwaka2004,na kusajiliwa mwaka 2008,lakini hadi sasa ina vyumba vya madarasaviwili,wanafunzi wapo 584,walimu walikuwa watatu,na mwaka huu mwezi oktobawameongezeka wanne na madawati ni 19 tu.Mwalimu Mwanamiwa aliongeza kwamba hali ya wanafunzi jinsi wanavyosoma nisana hasa ukizingatia kuwa wakati mwingine wanafunzi wanapeana zamu yakusoma ndani ya darasa moja,ikiwa ni darasa la kwanza na la pili kwa wakatimmoja ndani ya darasa moja.

Alisema njia nyingine ambayo huwa anaitumia katika kufundisha wanafunziwengine wanawekwa nje chini ya miti na kwamba vimetengenezwa vibao mithiliya mbao za semina na wanafunzi hufundishiwa.Aidha alisema kipindi cha masika kama hiki pindi inaponyesha mvua wanafunziwanaosomea chini ya miti hulazimika kuja madarasa ambao yamejengwa kwamsaada wa TASAF,na kujificha na hali hiyo ikitokea wale wanafunzi ambaowalimu wakisoma madasa yao yanakufa kwani kila chumba hujaa wanafunzi nakufikia hata 292.Mwalimu Mwanamima aliongeza kuwa hadi sasa shule hiyo ina darasa kwanza hadila sita na kutokana na hali hiyo inamuumiza kichwa pale wanafunzi watakaoingia darasa la saba namna watakavyofaulu na upande wa vyumba vyamadarasa upungu ni mkubwa kwani anahitaji vyumba vingine zaidi 7.

Akizungumzia changamoto nyingine mbali ya walimu mwalimu, huyo alisema mbaliya upungufu wa walimu,vyumba vya madarasa navyo bado ni tatizo kwani vyumbavitatu vya madarasa vya zamani, viliyoezekwa kwa makuti vinavuja sanakipindi cha masika kiasi ambacho wanafunzi hawawezi kusomea na vyumba hivyovya madarasa hutumika kipindi cha kiangazi.Alisema changamoto nyingine ni matundu ya vyoo ambapo kwa sasa matunduyaliopo ni 6,na hutumika kwa wanafunzi hao 584, ambapo mahitaji ni matundu31, pamoja na vitendea kazi ikiwemo vitabu.

Katika hotuba yake huku akishangazwa na hali hiyo,mkuu wa wilaya yaUyui,mkoa wa Tabora, Stanley Kolimba alisema ni hali ya ajabu kiasi kwambaimemsikitisha sana hasa katika kipindi hiki serikali imeamua kuvalia njugasuala la elimu kwa watoto wa kitanzania.Katika maagizo yake mkuu huyo wa wilaya aliagiza mwenyekiti wa kijiji hichokipya,kesho,kuitisha mkutano na wananchi wake na kupanga mikakati ya namnagani watakavyo jenga vyumba vya madarasa,na nyumba za walimu.

"Nimeshangazwa na taarifa ya upande wa elimu ;sasa hapa naagiza mwenyekitiwa kijiji kesho itisha mkutano na wananchi wako halafu mjadili namnamtakavyochangishana fedha ili zipatikane fedha za ujenzi wa vyumba vyamadarasa na nyumba za walimu na ikiwezekana niiteni nami nishiriki na yuelaambaye hatachangia nitamweka ndani." alisema.

Alisema shuel hiyo ataivalia njuga,hadi kieleweke,na kwamba kwa upande wake alichangia sh 500,000,na kwasihi wananchi hao kila mwananchi achangie kwanihakuna mtu atayekuja toka nje ya Tabora kuwajengea shule hiyo. Alisema serikali kwa sasa imevalia njuga elimu kwa kutenga bajeti kubwa nakwamba mwaka huu Uyui katika wilaya za Tabora imependelewa kwani imepewawalimu zaidi 420 hivyo ni wazi kwamba elimu wilayani humo inahitaji kutiliwamkazo.Akizunguymzia sikukuu ya Uhuru na Jamhuri,mkuu huyo wa wilaya alieleza maanayake na kutaka uhuru utumike katika kujiletea maendeleo,hasa katiak kilimona elimu.Hata hivyo aliwakumbusha wananchi katika kilimo kutumia mvua hzi kwa sasakwani tafiti zinaonyesha kuna uwezekano mvua zikawa chache msimu huu wakilimo na kutaka wananchi kuwa makini na kupanda mazao yanayovumilia ukame."Uhuru maana yake ni kutumia vyema nafasi za kujiletea maendeleo na kazikubwa iwe kwenye kilimo na elimu;...hii itawasaidia sana kufika hukotuendako." aliongeza.


No comments: