Wazungu Tanga kukamatwa,
Dar je?, Mpaka uswazi kibao!
WAKATI Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Meja Jenerali Mstaafu, Said Kalembo, akitangaza kula sahani moja na Wazungu wanaorandaranda mitaani hovyo bila shughuli maalum na kuwakamata katika Mkoa huo, hapa jijini Wazungu kibao wametapakaa katika mitaa ya uswahilini kiasi cha kupishana nao kama majirani tena katika mitaa ambayo huzanii kukutana nao.
Kamera ya Sufianimafoto leo ilifanikiwa kuwanasa wazungu hao wakiingia katika Mgahawa wa Uswazi huko mitaa ya Mkwajuni Hananasifu, huku wakiwa wamepiga pensi zao na mmoja akiwa ametinga malapa chini, huku wakipiga stori na kuzama katika mgahawa huo uliopo Barabara ya Katumba karibu kabisa na barabara kubwa ya Kawawa.
5 comments:
Sasa huu ni ubaguzi, kwanini wazungu??? Mna uwivu nao? Anzeni na Wahindi kama mnataka ubaguzi hao ndio maadui wakuu na wezi waharibifu wanaoishi nchini kwa mission tu na ndio chanzo cha rushwa.
Acheni ubaguzi bana kwani wazungu wakikatiza uswahilini na wakivaa malapa nini kinapungua? Mbona kuna waafrica kibao ulaya wanaranda tu.. nyie hamjui uchungu wa ubaguzi
kwakweli hapo sasa tutaanza ubaguzi,,mbona wahindi kibao na wachina wanauza maduka kariakoo hawakamatwi kama wana vibali vya kuwa hapo kihalali si walipewa na mamlaka husika leo mkiwakamata mnasema nini kuhusu izo mamlaka?kwani kula chai kibandani na kuvaa ndala kosa la jinai? mbona wa tz wengi wanatembea peku..sielewi kabisa
Acheni ubaguzi wabongo. Huku ulaya wa Afrika kibao wanazurura mjini masaa yote na hakuna anae wabagua?
Tena wengine wanatafuta makopo kwenye mandoo ya taka, je halali yao?
Mie naishi uswazi bongo, je, nikija na mume wangu mzungu halafu akaenda kwa mama ntilie banda la jirani kununua mihogo na mbilimbi hivi atakuwa kavunja sheria ya nchi?
mmewahi kuishi sehem mkabaguliwa? Huwa inauma tena usiombe.
Kama hao wazungu wapo kinyume na sheria basi acheni mamlaka zifanye kazi yake.
Huyu mkuu wa Mkoa ni Mjinga na hajui analofanya na wala hajui sheria za Uhamiaji ambazo ni za Kimataifa[Mtu anaruhusiwa kwenda popote dunia ili mradi anafuata sheria za uhamiaji wa nchi anayokwenda].Kwahiyo kama hao wazungu wapo hapo kihalali wanahaki wakutembea popote wanapotaka na kama wapo kinyume cha sheria za uhamiaji ndipo wachukuliwe hatua za kisheria.Mkuu wa Mkoa acha siasa za Kibabe tumia sheria.
Post a Comment