Sunday, December 26, 2010

Rais Jakaya Kikwete amteua
Jaji Mohamed Chande Othman
kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

Jaji Mohamed Chande Othman

Rais Jakaya Kikwete amemteua Jaji Mohamed Chande Othman kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Kuanzia 28 Desemba 2010.

Jaji Othman anachukua nafasi ya Jaji Brigedia Jenerali (Mstahafu) Agostino Ramadhani, anayestahafu kwa mujibu wa sheria kuanzia 27 Desemba 2010.

Jaji Othman alizaliwa 1.Januari 1952. Ana shahada ya kwanza ya sheria (LLB) toka Chuo Kikuu Dar es Salaam na shahada ya uzamili ya sheria (LLM) toka Chuo Kikuu cha Webster, Geneva Uswissi.

Jaji Othman amewahi kuwa Makamu Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Rwanda mjini Arusha na amewahi kushika nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali wa Timor ya Mashariki.

Jaji Othman amewahi kufanya kazi ndani na nje ya nchi katika Masharika mbalimbali ya kimataifa, kama vile Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Shirika la Msalaba Mwekundu Duniani.

Jaji Othman ataapishwa kesho Jumatatu tarehe 27 Desemba 2010 kwenye viwanja vya Ikulu saa 4 asubuhi.

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa habari msaidizi wa Rais,
Ikulu,
Dar es Salaam
26 Desemba 2010


No comments: