Sunday, December 26, 2010

Norway

Nafasi za mafunzo ya kijasusi


Maelezo ya nafasi za kazi
Idara ya ujasusi ina nafasi kadhaa za wanaotaka kuwa majasusi. Kazi ya jasusi itakuwa kutafuta habari 
kwa njia ya mawasiliano na watakaokuwa na uwezo wa kuchanganyika na watu wengine kwa kutafuta habari. Watakaohitimu wawe tayari kufanya kazi nje ya nchi.

Idara inatafuta wafanyakazi kwa kazi maalum. Watakaofuzu na kuwa wataalamu watatakiwa kufanya kazi kwenye idara kwa muda mrefu. Idara i
nataka wanafunzi wenye hulka nzuri kwenye jamii. Wagombea watakaofuzu kazi lazima wafanye kazi kwa bidii na kwa kujitegemea, na watakuwa sehemu ya timu maalumu. 

Waombaji lazima wawe wamemaliza mafunzo ya msingi wa kijeshi. 
Waombaji lazima wawe na nia ya kutumikia katika kazi za kimataifa, na kufanya kazi katika Kikosi cha Upelelezi kambi ya Setermoen iliyoko Troms.


Maelezo ya mchakato wa uteuzi
Juu ya maombi, wagombea watakaopita mchakato wa awali, watajulishwa juu ya mchakato wa uteuzi kwa ajili ya mafunzo. 
Watakazofuzu mchakato wa uteuzi huu, watapewa nafasi ya juu ya elimu ya msingi ya ujasusi na kupata nafasi kufanya kazi zaidi kwenye Kikosi cha Upelelezi.

Elimu ya msingi ya ujasusi huanza mapema Agosti 2011 na itaendelea kwa nusu mwaka. 
Mafunzo ya msingi ni ya lazima na mwanafunzi anatarajiwa kufanyakazi wakati mwingine jioni na wikiendi. Mafunzo yatalenga katika ujuzi wa vitendo, kijeshi na akili. Mafanikio ya kozi yanategemea sana motisha ya mwombaj, utulivu wa akili, uwezo kwa kuchanganyika kwenye jamii, tabia nzuri na uwezo wa kujifunza.

Elimu ya ujasusi, maendeleo ya binafsi na mafunzo ya kijeshi ni sehemu kuu ya maisha ya kila siku, wakati mwombaji asipokuwa kwenye kazi maalumu.

Waombaji lazima:

- atimize miaka 25 itakapofika mwaka 2011
- amepitia na kuhitimu mafunzo awali ya kijeshi
- awe na leseni ya udereva daraja B angalau miaka 2
- ajue kuzungumza na kuandika Kiingereza na Kinorwe
- amudu kukimbia mita 3000 chini ya dakika 14, aweze kupiga push-ups 25, hang-ups 4 na sit-ups 30
- asiwe na dosari zozote za kiusalama
- mwombaji akidhi mahitaji ya afya yake kwa ajili ya shughuli za kimataifa.

Maombi lazima yawe na:

- Sababu za msingi za maombi
- Tawasifu
- picha ya pasipoti/ picha ya mwombaji
- CV, na anwani ya barua pepe inayotumika
- wadhamini au marefarii wawili (kuhusiana na kazi)
- Nakala ya kauli ya hudumakazi, stashahada, vyeti, nk
- Ambatanisho linaweza kuwa kwenye fomati ya Doc au fomati ya  PDF na  picha iwe kwenye fomati ya jpeg.

Maombi lazima kutumwa kwa njia ya barua pepe kwa: rekruttering.ebn.mi@mil.no

Chanzo: http://www.finn.no/finn/job/fulltime/object?finnkode=25966732


No comments: