Monday, June 13, 2011

Balozi Mzale kukutana na Watanzania mjini Oslo


Balozi Mohammed Mzale.


Chama Cha Watanzania Oslo kinawataarifu kuwa balozi wetu mpya kwenye nchi za Nordic na Baltics, Mheshimiwa Mohammed Mzale anatarajia kuja Oslo kujitambulisha rasmi kwa serikali ya Norway. Pia ameomba kukutana na Watanzania Alhamisi tarehe 16 Juni 2011, mahali Pilstredet 48 (Høgskolen i Oslo) saa 10 na nusu jioni (16.30 CET) Watanzania wote mnakaribishwa. 

Tadhali sambaza taarifa hii kwa wengine.

No comments: