Wednesday, June 29, 2011

Hajaoga kwa miaka 37 !!!

Kailash Sinhg ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 65 hajawahi kuoga wala kukata ndevu zake tangu alipooga kwa mara mwisho kabla ya sherehe ya harusi ya kumuoa mkewe, mwaka 1974.

Singh anaelezea sababu ya msimamo wake huo kuwa ni sharti la utabiri aliopewa na mmoja wa kiongozi wa dini ya Hindu kuwa atakapopata mtoto wa kiume, basi mtoto huyo atakuwa mwenye mafanikio makubwa sana kwenye maisha yake na atakuwa tajiri sana.

Ni miaka 37 imepita lakini Singh anaendelea na msimamo wake wa kutooga mpaka pale atakapofanikiwa kupata mtoto wa kiume.

Singh ana jumla ya watoto saba wa kike lakini juhudi zake zote za kupata mtoto wa kiume bado hazijazaa matunda.

Mkewe ambaye sasa ana umri wa miaka 60, alishawahi kujaribu kuweka mgomo wa kutoa unyumba mpaka Singh atakapooga lakini mgomo huo uligonga mwamba kwani Singh hakujali chochote na matokeo yake mgomo huo uliisha.

Majirani na watoto wamekuwa wakimtania na kumtupia maneno ya kejeli mzee Singh ambaye amekuwa akipuuza kila anachoambiwa mpaka pale ndoto yake ya kuwa na mtoto wa kiume itakapotimia.

Familia yake nayo imewahi kujaribu kutumia maguvu kumuogesha kinguvu Singh kwenye mto lakini Singh alifanikiwa kuwazidi nguvu na kukimbia akisema kuwa ni heri afariki kuliko kuvunja sharti litakalomwezesha kupata mtoto wa kiume.

Kinachomfanya Sing awe anatoa harufu kali ni kazi yake ya ufugaji ambayo huifanya akizunguka kuwalisha majani ng'ombe wake kwenye kijiji chake cha Chatav ambapo hali ya hewa yake ni ya joto kali wakati mwingine kufikia joto la nyuzi 47C.

Mbali ya kutooga, Sing hajazikata ndevu zake na wala kuzinyoa nywele zake ambazo hivi sasa zimefikia urefu wa mita 1.9.

Ili kuusafisha mwili wake, Singh huota moto kila siku jioni huku akisali kumuomba mungu wake wa Kihindu, Shiva.

'Wakati ninapoendesha baiskeli kwenda kwenye shughuli zangu, watoto wamekuwa wakitania na kunipiga kelele kuwa siogi,hawaelewi kwanini nafanya hivi sitabadili uamuzi wangu mpaka nitakapopata mtoto wa kiume", alisema Singh.

No comments: