Thursday, June 30, 2011

Mnorweji wa kwanza kukimbia mita 100 kwa sekunde 9,99

Jaysuma Saidy Ndure.

Jaysuma Saidy Ndure amevunja rekodi ya Norway ya mita 100 kwa sekunde 9,99 kwenye Golden League iliyofanyika Lausanne, nchini Uswiss leo jioni. Kwenye mbio hizo, Jay alikuwa wa tano. Asafa Powell wa Jamaica alikuwa kwa kwanza kwa sekunde 9,78, akifuatiwa na Mjamaika mwenzake, Michael Frater (9,88) na Mfaransa Christophe Lemaitre (9,95). Jaysuma Saidy Ndure ni Mnorweji mwenye asili ya Gambia.

No comments: