Thursday, June 30, 2011

Oslo

Wanaijeria 14 wafukuzwa Norway

Waziri wa sheria wa Norway, Bw. Knut Storberget leo kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Jana jioni Wanaijeria 14 wamerudishwa kwao kwa nguvu. Kati ya hao, 9 wana makosa ya jinai zaidi ya 50. Haya yametangazwa na waziri wa sharia, bw. Knut Storberget kwenye mkutano na waandishi wa habari. Kufukuzwa huku kwa hao Wanaijeria ni moja ya mpango wa Norway uitwao Frontex, ikishirikiana na nchi za EU. Makosa megi ya Wanaijeria hao ni ya jinai, wizi na kuingia nchini Norway kwa hati bandia za kusafiria.

Ndege hiyo iliyoondoka na Wanaijeria hao, ilitua Sweden, Denmark, Ujerumani, Hangari (Hungary) na Ufaransa kuchukua Wanaijeria waliofukuzwa katika nchi hizo.

1 comment:

Anonymous said...

aisee hii kali ,lakina jamaa hawa noma