Sunday, July 03, 2011

Kauli ingekuwa nauli, tungeshapanda basi la kwenda kwenye raha tupu...

Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.


Mpenzi Frank,

Mambo mpenzi? Mimi mzima, lakini ngoja nianze kwa kukusuta. Nilifikiri una sababu maalaum, kumbe umeambukizwa na ugonjwa wa kitaifa. Kila siku nakuambia ufanye maamuzi magumu, eti ukubali kumwoa Hidaya wako anayekupenda kufa na kupona lakini wewe wabaaaana utadhani serikali. Huwezi kuamua? Tena upande wako wala si maamuzi magumu na hautajuta hata siku moja.
Lakini naendelea kusubiri mpenzi wangu. Kama serikali inaweza kusitasita kwa nini usisite na wewe teh teh. Na usiwe na wasiwasi, sikutii shinikizo. Afadhali hata wewe uliye na mpango wa maisha. Tuna malengo yetu na najua unafanya juu chini kufikia haya malengo licha ya matatizo yote yanayotukabili. Siyo mambo ya kukurupuka hapa na kupukutika pale. Angalau na sisi tunapima kabla ya kufanya maamuzi yetu….bofya na soma zaidi>>>>>

No comments: