Friday, July 01, 2011

Unaweza kupiga kura yako ya uchaguzi wa serikali za mitaa na mikoa kuanzia leo Julai MosiKuanzia leo Julai Mosi, unaweza kupiga kura yako kwenye kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na za mikoa hadi Septemba 9, mwaka huu. Uchaguzi wenyewe ni 11 na 12 Septemba mwaka huu. Kwenye hizi kura za sasa hivi mtu anaweza kupiga kura kwenye kituo chochote cha uchaguzi hadi Septemba 9. Mpiga kura anatakiwa kuwa na kitambulisho kitachotambulika kama kadi ya benki, leseni ya gari ama pasipoti.

Mtu yeyote ambaye amekaa Norway miaka 3 na kuendelea hata kama hana uraia wa Norway anaweza kupiga kura kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa na za mikoa.

Kwa maelezo zaidi angalia:http://www.regjeringen.no/en/dep/krd/kampanjer/election_portal.html?id=456491 

No comments: