Saturday, August 06, 2011

Luteni Jenerali Silas Mayunga “Mti Mkavu” afariki dunia


Luteni Jenerali Silas Mayunga "Mti Mkavu" (Kushoto) na Jenerali David Musuguri  "Kambale"(kulia) wakipokelewa mwaka 1979 kwa heshima baada ya kumng´oa nduli Iddi Amin madarakani nchini Uganda.

Kwa taarifa za uhakika zilizopatikana kutoka nchini India kuwa mpiganaji wetu shupavu na kiongozi mwadilifu, Luteni Jenerali Silas Mayunga “Mti Mkavu” hatuko naye tena, amefariki leo katika hospitali ya Apollo New Delhi, India ambako alikuwa amelazwa tangu mwezi, Julai 2011.

Jenerali Mayunga atakumbukwa kwa mengi kwa jinsi alivyotumikia Taifa letu kwa utumishi uliotukuka, atakumbukwa daima kwa jinsi alivyoongoza mapambano ya vita vya Kagera kumng'oa Nduli Idd Amin. Alijipatia jina maarufu la MTI MKAVU alipokuwa kwenye vita ya Kagera kwa jinsi alivyokuwa akishika na kuuegemea mti mkavu kila alikoenda, wakati wa vita ya Kagera 1978-1979.

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema.
RIP.

1 comment:

Anonymous said...

R.I.P Jenerali Mti Mkavu