Thursday, August 18, 2011

Uteuzi:Rais Jakaya Kikwete Amteua Bwana Msafiri Wilbert Marwa kuwa Mwandishi wa Hotuba Msaidizi wa RaisRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatano, Agosti 17, 2011, amemteua Bwana Msafiri Wilbert Marwa kuwa Mwandishi wa Hotuba Msaidizi wa Rais. Uteuzi huo unaanza mara moja.

Kabla ya uteuzi wake, Bw. Marwa alikuwa Ofisa Mambo ya Nje Mwandamizi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Bw. Marwa (39) alijiunga na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Januari 1999 na tokea Agosti 2004 alifanya kazi katika Ubalozi wa Tanzania mjini Addis Ababa, Ethiopia kabla ya kurejea nyumbani mwaka jana.

Bw. Marwa ana Shahada ya Kwanza ya Biashara (Bachelor of Commerce) kutoka Chuo Kikuu cha Mysore, India na Diploma ya Juu kutoka Kituo cha Centre for Foreign Relations cha Dar es Salaam.
Imetolewa na: 

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu,
DAR ES SALAAM.
17 Agosti, 2011

No comments: