Monday, September 12, 2011Chama Cha Watanzania Oslo
Simu ya kiganja: +47 908 06 901
Oslo,
Norway.Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
IKULU,
Dar es Salaam.KUHUSU: SALAAM ZA RAMBIRAMBI

Sisi Watanzania tuishio Oslo na vitongoji vyake, tumeshtushwa na kusikitishwa na ajali ya kuzama kwa meli ya MV. Spice Islander kuamkia tarehe 10 Septemba 2011 na kusababisha Watanzania wenzetu kadhaa kupoteza maisha yao na wengine kuumia.

Kwa niaba ya Watanzania tuishio Oslo na vitongoji vyake, Chama Cha Watanzania Oslo, kinatoa salaam za rambirambi kwa Watanzania wote, ndugu, jamaa na marafiki wa waliofiwa au kuhusika kwa njia moja ama nyingine kwenye ajali hiyo.

Dr. Tito Sendeu Tenga,
Mwenyekiti,
Chama Cha Watanzania Oslo.

No comments: