Sunday, September 25, 2011

Little Brother Is Watching You!


Ghafla hivi karibuni, kompyuta yangu imeanza kuwa na huruma na mimi. Imeanza kuniuliza maswali ambayo sihitaji kuingia Facebook kuyaona. Maswali kama vilie, umri wangu na tarehe za kuzaliwa za marafiki zangu.

Facebook wanajua umri wangu na wa marafiki zangu. Google wanajua saa zote niko wapi, na natafuta nini au navinjari wapi kwenye mitandao. Inajulikana kuwa Google, Yahoo! na zingine zinashirikiana na wabia kuwapa habari za wateja wanaotumia huduma zao.

Inawezekana kabisa kuwa pamoja na kuwa kompyuta yangu inalindwa kama Fort Knox, lakini labda kuna upenyo ambao wajanja wanautumia kunichungulia!

Kitu ambacho wateja wengi wa simu za viganja za kisasa (smartphones) hatutilii maanani ni vijiprogramu (Applications = Apps) tunavyovifyonza sisi watumiaji w simu hizo. Nyingi ya hivi vijiprogramu ni bure bileshi au vinauzwa kwa bei ya chee!

Je, wanaobuni na kuzitengeza hizo Apps wanapataje faida?

Hawa jamaa, mapato yao yanapatikana kwa kushirikiana na wabia wao, au wafanya biashara za kwenye mitandao. Tunapofyonza Apps, habari zetu zinahifadhiwa kwenye hizo Apps. Habari kama; anwani zetu, anwani za marafiki zetu na si ajabu hata nywila zetu tunapofungua hizo simu.

Vijiprogramu hivi, vinaundwa kutoka "systems" za kampuni ya Flurry ya Marekani. Flurry wanakusanya habari nyingi sana kiasi ambacho "database" yao, inahifadhi kwenye Petabytes*. Hivi karibuni, Flurry wamesema kuwa wameanza kuhifadhi kwenye Exabytes*.

Tumezoea kujiuliza au kusoma kuwa "Big Brother Is Watching You!" Lakini jinsi hii teknolojia inavyokwenda kasi, lazima pia tuwe waangalifu na Little Brother.

Hivi kwa nini kiprogramu mfano cha tochi...unakifungua halafu, unakiwasha ili kiwe tochi, ghafla kuna kidaka sauti kinafunguka ambacho wewe hukijui. Kwa nini?

"Little Brother Is Watching You!"

Nawatakia wikiendi njema!


Mwamedi Semboja,
Oslo.

2 comments:

Anonymous said...

Semboja,

umekuwa paranoid usiogope sana

Semboja said...

Hapana si kuwa paranoid. Ni ukweli mtupu!