Monday, September 26, 2011


Wangari Maathai “Mama Mti”
afariki dunia


Profesa Wangari Maathai (71) mpigania haki za kuhifadhi mazingira (mwanamazingira) amefariki jana usiku hospitalini mjini Nairobi. . Imeripotiwa kwenye televisheni za Kenya; Citizen TV na NTV kuwa Maathai amefariki kwa ugonjwa wa saratani (kansa). Wangari ni mwanamke wa kwanza Afrika Mashariki na ya kati kupata shahada ya uzamivu (Ph.D) pia ni mwanamke wa kwanza Mwafrika kupata tuzo ya amani ya Nobel mjini Oslo mwaka 2004. Mwenyezi Mungu Amweke Pema...Ameen!

No comments: