Wednesday, October 26, 2011Hatarini kufungwa kwa
kusoma barua pepe ya mkewe.Walker Leon (33) wa Rochester Hills jimbo la Michigan nchini Marekani anaweza kufungwa miaka 5 jela akikutwa na hatia mahakamani ya kufungua na kusoma barua pepe ya mkewe. Walker alianza kuwa na mashaka na mkewe; Clara Walker kuwa anafanya ugoni. Akaingia kwenye barua pepe ya mkewe kwa kutumia jina tumizi na nywila ya mkewe na akathibitisha mashaka yake ya kuwa mkewe alikuwa na mwanamme wa nje. Walker alipomvaa Clara kwa ugoni wake; Clara akajibu mapigo kwa kumshtaki mumewe. Kesi iko mahakamani na kama Walker akikutwa na hatia, kifungo chake ni miaka 5

Inasemekana asilimia 45 ya wanandoa wanachunguliana barua pepe zao.


No comments: