Wednesday, October 26, 2011

Dar es Salaam


Kuhusu gazeti la MwanaHalisi


Habari nilizozipata kupitia mtandao wa nchi kavu kuhusiana na Gazeti la Mwanahalisi ambalo huwa linatoka kila wiki siku ya jumatano ni kua wiki hii halijajatoka huku mikoani hakuna hata matumaini ya kulipata wiki hii kama wanavyosema wauza magazeti. Na habari nilizopata ni kua tokea mzee wa Monduli kuongea na wanahabari kua atafanya kitu mbaya kupitia kwa wanasheria wake kama magazeti kuandika habari za kumuhusu yeye binafsi, sasa umbea uliopo ni kua gazeti hili la Mwanahalisi lilikua limesheheni habari za kutikisa nchi kuhusina na bwana huyu, imebidi bwana Saidi Kubenea na jopo lake walifanyie Editing gazeti lao kuhusiana na habari zilizokua zinamuhusu mkulu huyu na ndio maana mpaka sasa haliko hewani. Jamani naomba kuwakilisha na mtupe dondoo kama hili gazeti kuna mtu kalipata leo hii.

Kutoka Jamii Forums na
Mdau,

Jamaldeen Mazar E Shariff Bin Ad-Din Vituz Mamluk Ibn Zenjibari

No comments: