Saturday, October 29, 2011

Majira ya theluji


Saa 9 usiku kuamkia Jumapili, 30 Oktoba 2011, hapa Norway (Skandinavia) tunabadili majira na kuingia majira ya theluji (Winter time). Kufuatia na mabadiliko ya majira, tunarudisha saa moja nyuma. 

Tuna tofauti ya masaa mawili na saa za Afrika Mashariki kwenye majira ya theluji. 

Mfano:

Hapa Norway ikiwa saa 4 za asubuhi,
Tanzania (Afrika Mashariki) ni saa 6 za mchana... 

Mabadiliko ya saa hufanyika mara mbili kwa mwaka.


Jumapili ya mwisho ya Machi, kuingia majira ya Kiangazi (Summer). Tunasogeza saa moja mbele. Tofauti ya saa moja na Afrika Mashariki.


Jumapili ya mwisho ya Oktoba, kuingia majira ya theluji (Winter). Tunarudisha saa moja nyuma. Tofauti ya masaa mawili na Afrika Mashariki.


No comments: