Sunday, October 30, 2011

Aftenposten:
licha ya hela za misaada kupotelea kwa wajanja;
Norway yamwaga mahela Tanzania.

Habari hizi zimeandikwa kwenye gazeti la Jumamosi 29 Oktoba 2011 la Aftenposten (ukurasa wa 23, 23, 25, 26 na 27), zikiwa na kichwa cha habari “Verden sett fra Tanzania”
Wakati Norway inafanya majadiliano na Serikali ya Tanzania juu ya kurudishwa mamilioni ya hela za misaada yaliyopota bila kujulikana; Waziri wa misaada wa Norway; Bw. Erik Solheim amwaga kroner milioni 500 kwa Tanzania kwenye mradi ulioanzishwa na Umoja wa mataifa kuungwa mkono na waziri mkuu wa Norway; Bw. Jens Stoltenberg uitwao “REDD – Reducing Emissions for Deforestation Degradation. Nchi ambazo zitanufaika sana na REDD ni Brazil, Tanzania, Indonesia, Guyana, Mexico na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Kwenye mradi uitwao “Management of Natural Resources Programme (MNRP)” Norway ilitoa kroner milioni 300. Hela hizo zilitolewa katika kipindi cha mwaka 1994-2006. Novemba 2006; Brian Cooksey alitoa ripoti ya miaka 12 ya misaada nchini Tanzania ambayo ilionyesha kuwa kulikuwa na utata na kupingana na ripoti zilizokuwa zikitolewa na Wizara ya Mali Asili na Utalii. Cooksey aliona utata wa ripoti ya wizara hasa kwenye mradi kwenye kisiwa cha Mafia (MIMP). Mwezi Mei 2007 ripoti ya mwisho kuhusu mradi kwenye kisiwa cha Mafia, ulifichua ufisadi wa mradi huo; kuwa kuna mahela kibao yameliwa. Mkaguzi Mdenish Arthur F. Andreasen ndiye aliyetoa ripoti ya ukaguzi hakiki ya mradi wa huo kuwa mahela yameliwa!

Pamoja na hayo yote; ya kuwa Tanzania imekuwa ikipokea misaada mingi kutoka nchi za Magaharibi hususan Norway na kuwa idadi kubwa ya misaada hiyo imekuwa ikipotea kwenye mifuko ya wajanja; Aftenposten wanashangazwa na uamuzi wa waziri wa misaada; Bw. Erik Solheim kuendelea kumwaga mahela nchini Tanzania.

1 comment:

Anonymous said...

Kazi kwelikweli mwisho na wenyewe watakasirika watulazimishe tuoane jinsia moja,pesa za jenga mahekalu dar!