Monday, October 31, 2011

Molde FK mabingwa wa soka wa NorwayTimu ya soka ya Molde FK imenyakua ubingwa wa soka ligi kuu ya Norway jana baada ya kutoka sare na Strømgodset ya Drammen 2-2.

Molde FK imenyakua ubingwa kwa kumalizia na pointi 55, wakati mshindi wa pili; Tromsø wamemalizia na pointi 47 na Rosenborg ya tatu na pointi 46.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Molde kuwa mabingwa wa soka hapa Norway. Molde katika msimu huu ulioisha jana imekuwa ikifundishwa na mchezaji wa zamani wa Manchester United; Ole Gunnar Solksjær.

No comments: