Thursday, November 10, 2011


Hii ilitotokea Dar es Salaam,
miaka ya sabini.


Kuna moja ilitokea miaka ya 70 maeneo ya Kariakoo, Dar es Salaam. Enzi hizo sinema za Empress, Empire, Avalon etc...zipo.

Kuna jamaa mmoja alitoka jioni akajiendea sinema Empire. Wakati yuko kwenye foleni ya tiketi akamwona dada mmoja mzuri. Jamaa akaamua kumfuata na kumtongoza yule dada. Yule dada hakufanya hiana; akaonyesha dalili za kumkubalia jamaa. Jamaa akamkatia yule dada tiketi wakaaingia na kuangalia sinema.

Baada ya sinema kumalizika; yule dada akaamua kumwondoa wasiwasi yule jamaa kuwa hamdanganyi kuwa siku ya pili (Jumapili) watakutana. Yule dada akatoa mkufu wake akampa yule jamaa na yule jamaa alikuwa amevaa koti flani hivi akampa yule dada. Yule dada akamwelekeza yula jamaa mahali anapokaa Kariakoo. Wakagana. Jamaa alikuwa anakaa Magomeni.

Siku ya pili ilikuwa Jumapili, jamaa akajifungasha huyooo na safari hadi Kariakoo alikoelekezwa na yule dada.

Jamaa akabisha hodi akapokelewa. Jamaa akasema amemfuatana flani walikutana jana yake Empire Cinema. Mama mmoja aliyemfungulia mlango na watu wengine kwenye ile nyumba wakaanza kulia. Jamaa akashtuka, akawauliza kulikoni?

Wakamwambia mbona flani alishakufa siku nyingi? Jamaa hakuamini alidhani wanamdanganya.

Jamaa akatoa ule mkufu wa yule dada akawaonyesha. Wakazidi kulia na kumwambia ni kweli mkufu ni wa yule dada na ulikuwa ndani ya nyumba pale Kariakoo!

Yule mama (Mama wa marehemu) akaamua kumchukua jamaa hadi kwenye kaburi la binti yake.

Kufika kwenye kaburi; wakakuta juu ya kaburi, koti la yule jamaa.

Jamaa alizimia!

Na mdau;
Omari “Ommy” Guy Agallo Chichi

3 comments:

Nzo Ekangaki said...

Hii hata mimi niliisikia

Anonymous said...

Kweli Wantanzania miaka hiyo walikuwa GIZANI!! Kuweza kuamini Ushuzi huo!! Poleni!!

Dotto Mokili said...

Si kama walikuwa gizani...ni imani ya watu. Imani kitu kibaya sana. Inawezekana kweli ilitokea au ni uvumi tu hatuwezi kujua...