Thursday, January 19, 2012

Mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa Norway ajiuzulu


Jana usiku mkurugenzi mkuu wa idara ya usalama wa taifa ya Norway (PST = Politiets Sikkerhetstjeneste) Bi. Janne Kristiansen alijiuzulu, kufuatilia kuchemsha kwa kusema kuwa «Norway ina majasusi nchini Pakistan». Bi. Kristiansen alikuwa akihojiwa Bungeni juu ya tukio la ugaidi lililotokea Norway Julai 22, mwaka jana na kuhusu PST kushindwa kuona au kugundua kuhusu tukio hilo la ugaidi. Mkurugenzi msaidizi; Bw. Roger Berg anakaimu nafasi hiyo.Read more: News in English 

No comments: