Kibaka aiba
iPhone akamatwa kwa kutumia “Find My iPhone”
Jamaa aliibiwa iPhone yake ana akawapigia
polisi kuwa kaibiwa iPhone yake. Kwa kupitia “application” iitwayo “Find My
iPhone” polisi hawakuwa na kazi ngumu ya kumkamata kibaka wa iPhone ya jamaa!
“Find My iPhone” ni app ambayo unaweza
kuingia kwenye iPhone yako kupitia kwenye kompyuta, halafu ukawa unaweza kufuta
programu zilizoko kwenye iPhone au kujua kwa uhakika kabisa wapi iPhone yako
iko kwa kutumia ramani.
Tukirudi kwenye tukio hilo lililotokea
Jumamosi ya leo, jamaa aliyeibiwa simkono (simu ya mkononi) aliwapigia polisi
na kuwaambia kuwa kwenye iPhone yake kuna “Find My iPhone” na anajua wapi iko
na angewaongoza polisi kwa mwizi huyo. Polisi walikubali kufuatana na jamaa
huyo hadi hapo aliposema. Wakamkamata huyo kibaka na mfukoni kwake wakaikuta na
kuthibitisha ni iPhone ya jamaa. Kibaka amechukuliwa na yuko lupango, hatima
yake haijulikani.
Haya yamethibitishwa na na mkuu wa
operesheni wa kituo cha polisi cha katikati ya mji wa Oslo, Bw. Tor Jøkling.
Mwamedi Semboja,
Oslo.
No comments:
Post a Comment