Monday, March 26, 2012


Nasra Mohamed: Ukatili na unyanyasaji uliovuka mipaka


Hivi karibuni TBC1 wamerusha habari kuhusu tukio la ajabu sana, ambalo linahusisha ukatili wa hali ya juu. Nasra Mohamedi mkazi wa Bunda, Mara amelazwa hospitali ya Bugando baada ya mume wake kumfanyia vitendo vya ukatili wa kutisha. Huyo mama amesimulia kuwa mume wake alimgonga na gari na kisha akamburuza kwa mita kama 100 hivi. Amevunjika mbavu 7, mguu na ana vidonda vya kutisha sehemu mbali mbali za mwili. Pia sikio lake moja limekatika. Nasra amekaa ICU kwa siku 21 na sasa anaendelea vizuri. Hata hivyo, bado mume wake anamtumia vitisho kwamba lazima ammalize.


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia na watoto; Sophia Simba amemtembelea Nasra hospitali na kuomba polisi wamwongezee ulinzi. Amesema kuwa pamoja na kwamba mume wake Nasra ametoroka na haijulikani yuko wapi. Hata hivyo, polisi wataendelea kumsaka hadi wamkamate.


No comments: