Monday, March 26, 2012

Rais Abdoulaye Wade ashindwa uchaguzi Senegal

Abdoulaye Wade.


Rais Abdoulaye Wade wa Senegal amekubali kushindwa kwenye uchaguzi mkuu wa duru ya pili nchini humo uliofanyika jana Jumapili. Wade alimpigia simu Rais mtarajiwa Macky Sall kumpongeza kwa ushindi.

Sall aliwahi kuwa Waziri Mkuu kwenye serikali ya Wade, wakashindana kiitikadi.

Kukubali kushindwa kwa Wade ni hatua muhimu ya kidemokrasia barani Afrika, kwani ni aghalabu sana kwa Marais waliopo madarakani kuachia ngazi hivi hivi bila rabsha!

Rais wa kwanza wa Senegal; Léopold Sédar Senghor (9 October 1906 – 20 December 2001)alikuwa Rais wa kwanza barani Afrika kujiuzulu akiwa madarakani, Desemba 1980.

No comments: