Tuesday, July 03, 2012


Mwanamke mwenye asili ya Tanzania anatafutwa, ametoweka nyumbani
baada ya kudai kudundwa na mmewe

Mbwa wa polisi wakisaidia kwenye msako wa kumtafuta mwanamke mwenye asili ya Tanzania aliyepotea Tromøy, Arendal. Picha na Anne Karin Andersen (Agderposten)


Tromøy, Arendal (Norway).


Jana saa moja mwanamke mmoja alipiga simu polisi  na kusema kuwa amepigwa nyumbani kwake. Baada muda mfupi, akaonekana ametoka nyumbani kwake, maeneo ya Tromøy, Arendal. Ametoweka na hajaonekana tokea jana. Mwanamke huyo ana asili ya Tanzania.

Mumewe alitoa taarifa polisi baada ya kutoonekana kwa muda mrefu. Tokea jana amekuwa akitafutwa na helikopta, boti za polisi, polisi wenye mambwa, jamaa wa msalaba mwekundu na watu wa kujitolea.


Chanzo:Agderposten

No comments: