Tuesday, August 21, 2012

Dr. Peter Kafumu (CCM) aenguliwa Ubunge wa Igunga, Tabora

Dr. Peter Kafumu.

Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imetoa hukumu ya kesi ya ubunge iliyokuwa ikimkabili mshindi wa ubunge jimbo la Igunda Dk Peter Kafumu (CCM).Hukumu hiyo ya kupinga matokeo yaliyompatia ushindi Dk Kafumu imetolewa leo ambapo imemuengua mbunge huyo katika nafasi yake ya ubunge

Shauri hilo lilifunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Kashindye dhidi ya Dk. Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na msimamizi wa uchaguzi huo, Protace Mgayane.Shauri hilo lilianza kusikilizwa rasmi Machi 26 mwaka huu chini ya Jaji Mary Nsimbo Shangali.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya, Silvester Kainda, alisema kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora ilipanga hukumu hiyo isomwe Agosti 20 mwaka huu, lakini kutokana na tarehe hiyo kuangukia Sikukuu ya Idd, hukumu hiyo imesomwa Leo

Wakili wa mlalamikaji, Profesa Abdallah Safari, alizungumza kwa njia ya simu jana na kusema kuwa zaidi ya malalamiko 13 waliyawasilisha katika mahakama hiyo. 

 Alisema kuwa kulingana na malalamiko hayo, wanaiachia mahakama itatoa uamuzi wake kwa vile kila kitu wamekiwasilisha na kwamba ushahidi wote umesikilizwa.

Dk. Kafumu alitetewa na mawakili wawili, Anthony Kanyama na Kayaga Kamaliza. Mojawapo ya malalamiko katika kesi hii ni pamoja na vitisho vilivyotolewa na viongozi wa serikali,ahadi ya ujenzi wa daraja la Mbuntu pamoja na kugawa mahindi.No comments: