Wednesday, September 26, 2012



Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imekuwa na taarifa na malalamiko mbalimbali kuhusiana na mauzo ya vocha ya Tsh450 inayouzwa  kwa bei ya juu Tsh500 wakati vocha hizo kiuhalali zinauzwa kwa Tsh 450. Vocha hizi za Tsh450 zimetolewa katika soko ili kuwawezesha  wateja wetu kuwa na mawasiliano ya urahisi zaidi. Bei halali ya vocha hii ni Tsh450 kama ilivyo andikwa kwenye Vocha na tunawahimiza wateja wetu wanunue vocha hizo kwa bei halali iliyotangazwa,siyo vinginevyo.

Tunashukuru kwa maoni yenu juu ya hili swala na tunafatilia kwa ukaribu zaidi kwa wauzaji wa vocha hizi kuhakikisha wanatoa huduma bora na ya uhakika kwa wateja wetu na wananchi kwa ujumla.

Tafadhali shirikiana nasi kwa kutoa taarifmbalimbali hususani kuhusina na swala hili la vocha hizi za Tsh450 kupitia kurasa yetu ya facebook na Twitter.

No comments: