Thursday, September 27, 2012

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda asingoje kuzomewa tena

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

RAIS wangu, Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda, amesikika akilia hadharani na kusema: “Kwa kweli hali ya 17-9-2012, ilinitisha sana. Kama mimi nimezomewa, kiongozi gani atakayesalimika kuzomewa akienda uwanjani hapo?”

Aliyasema hayo baada ya kuzomewa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Sahara jijini Mwanza. Alipokuwa akiondoka msafara wake ulipopolewa kwa mawe! Hili hakulisemea!
Hatuwezi kukubali viongozi wetu wazomewe na kisha wafurumishwe kwa mawe kama vibaka. 

Wanaosababisha haya kutokea wawe wananchi, au wawe viongozi wenyewe lazima wadhibitiwe mara moja. Mashuhuda wanasema uwanja mzima ulizomea! Uwanja mzima ulikuwa umelewa? Wanaoweza kulewesha uwanja mzima sasa basi, hawatufai!


No comments: