Dr. Harrison Mwakyembe awafukuza kazi wawili bandarini
Dr. Harrison Mwakyembe
Waziri wa Uchukuzi
Dokta HARRISON MWAKYEMBE amewaafukuza kazi EPHRAIM MGAWE, na Naibu wake Bwana
JULIUS MFUKO kufuatia ripoti iliyotolewa na tume maalum ya kuchunguza hali ya
uendeshwaji wa bandari hiyo na kuonyesha kuwa watendaji hao wamekosa umakini pamoja
na kufanya uzembe uliopitiliza.
Akisoma ripoti
hiyo Dokta MWAKYEMBE amesema kuwa Viongozi hao wameshindwa kuonyesha umaridadi
wa kuisimamia bandari hiyo, hali iliyopelekea kuisababishia Hasara kubwa
Serikali sambamba na kushusha hadhi ya Bandari ya Dar es Salaam, hadi kufikia
hatua ya kutajwa kama Bandari isiyoingiza faida yoyote miongoni mwa Bandari 36
za barani Afrka.
Katika Hatua
nyingine Dokta MWAKYEMBE ametangaza kuwafukuza kazi Meneja Mkuu wa Bandari hiyo
KASSIAN NGAMILO pamoja na Meneja wa kitengo cha Mafuta CAPTAIN TUMAINI MASSAWE,
kufuatia kushindwa kusimamia ipasavyo mikataba mbalimbali ya uondoshaji wa
mafuta machafu bandari hapo sambamba na uzembe uliopitiliza.
Hata hivyo Dokta
MWAKYEMBE amebainisha kuwa Wizara yake haitamvumilia mtendaji yeyote kutoka
idara ama taasisi iliyo chini ya Wizara hiyo ambaye utendaji wake utaonekana
kulega lega, na kusabaisha Serikali kupata hasara pasipo sababu za Msingi.
Kufukuzwa kwa
Viongozi hao ni miongoni mwa utekeleza wa uboreshaji wa Bandari ya Dar es
Salaam ambayo imeshika nafasi ya Mwisho kwa uingizaji faida katika Bandari 36
za Bara la Afrika hii ni ikiwa ni Ripoti iliyotolewa hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment