Thursday, March 28, 2013

Mbunge wa Chama Cha Wananchi (CUF) Jimbo la Chambani, Salim Hemed Khamis afariki duniaMbunge wa Chama Cha Wananchi (CUF) Jimbo la Chambani, Salim Hemed Khamis afariki dunia, Mbunge huyo alianguka jana ghafla akiwa katika kikao cha kamati ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa katika ofisi ndogo za bunge jijini Dar es salaam wakati kamati hiyo ikiendelea na kikao chake.

Mbunge huyo ambaye siku za hivi karibuni ametoka nje ya nchi kwa matibabu ya afya yake amefikwa hali hiyo na kubebwa na baadhi ya wabunge kwa kushirikiana na baadhi ya wandishi wa habari kutolewa nje ya chumba cha mkutano na kupelekwa hospital ya taifa ya Mhimbili kwa uchunguzi na matibabu zaidi.


No comments: