Saturday, March 30, 2013

SummertimeSaa 8 usiku kuamkia Jumapili, 31 Machi 2013, hapa Norway (Skandinavia) tunabadili majira na kuingia majira ya kiangazi (Summertime). Kufuatia na mabadiliko ya majira, tunaongeza saa moja mbele. 

Tuna tofauti ya saa moja na saa za Afrika Mashariki kwenye majira ya kiangazi. 

Mfano:

Hapa Norway ikiwa saa 5 za asubuhi,


Tanzania (Afrika Mashariki) ni saa 6 za mchana... 

Mabadiliko ya saa hufanyika mara mbili kwa mwaka.


Jumapili ya mwisho ya Machi, kuingia majira ya Kiangazi (Summer). Tunasogeza saa moja mbele. Tofauti ya saa moja na Afrika Mashariki.


Jumapili ya mwisho ya Oktoba, kuingia majira ya theluji (Winter). Tunarudisha saa moja nyuma. Tofauti ya masaa mawili na Afrika Mashariki.


No comments: