Friday, May 24, 2013


Kuwaaga wanafunzi Watanzania wanaomaliza masomo yao 2013


Ndugu wanaTASAO kama ilivyo ada yetu ule muda wa kuwaaga wenzetu wanaomaliza masomo mwaka 2013 umewadia. Sherehe zitafanyika siku ya

Jumamosi ya tarehe 08.06.2013.

Sherehe hizi zitafanyika katika

Ukumbi wa NORBERG KIRKE

pale ilipofanyika sherehe ya Uhuru mwezi Desemba 2012. Sherehe zitaanza saa 12.00 jioni.

Tunaomba sana wote tushiriki kwa wingi.

Sambamba na hilo tunaomba kuwakumbusha michango ya kiingilio na ada ya kila muhula kwa wale ambao hawajatoa. Kwa sababu sherehe hizi zinaendeshwa kwa michango yaani kiingilio na ada tu hakuna mchango zaidi ya huo. Tunawaomba sana tujitume wenyewe. Unaweza wasilisha mchango wako moja kwa moja kwa kiongozi yeyote wa TASAO.

Naomba kuwasilisha.

Tunawasalimu pia wale wote mlio huko nyumbani Tanzania. Kila la kheri katika kujenga nchi yetu.
DEZIDERY KAJUNA


Chanzo: Tanzania Students Association Oslo (TASAO) http://tasao.blogspot.no/ 


No comments: