Friday, May 24, 2013

Wabunge wa CCM walipokutana na mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete


Mawaziri wa CCM wachambuana wenyewe kwa wenyewe


Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, Bw.Bernard Membe.

Bi. Hawa Ghasia; waziri wa nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia utumishi na serikali za mitaa.


Wabunge wa CCM wamemrarua waziri wa mambo ya nje Bernard Membe kuwa ni kinara wa fujo na vurugu zinazoendelea Mtwara.

Wa kwanza kuchangia alikuwa ni mbunge wa Newala, alisema Membe ni mtu hatari na ni kirusi Ndani ya chama kwani anamtumia mbunge wa Mtwara mjini Murji na misikiti kumchafua Waziri wa Serekali za Mitaa Hawa Ghasia, Baada ya Munde alifuata Hawa Ghasia ambaye naye alimshtutumu Membe kuwa anamfitini kwa kumtumia Murji, na Murji kupiga misikiti anaendesha mkakati kupitia misikiti ,''vurugu za mwezi Januari nyumba yangu pamoja na ya Mhe.Anna Abdallah zilichomwa moto Mhe mwenyekiti jana tena wamechoma nyumba yangu na ofisi za chama moto nimefanya utafiti nimegundua ni waziri mwanzagu ndie anaenifitini kwa wananchi wa Mtwara hii ni hatari sana kwa mustakabali wa chama na taifa kwa ujumla'

Waziri Ghasia alienda mbali zaidi kwa Kusema Kama vitega uchumi, Membe anavyo vya kutosha Mtwara lakini hazichomwi wala hazirushiwi mawe,hii inasikitisha.No comments: