Tuesday, July 30, 2013

Reginald Mengi - Nchi inanuka rushwa!



MWENYEKITI wa kampuni za IPP, Reginald Mengi ametoboa siri kuwa hakuna mfanyabiashara wa Tanzania aliyefanikiwa katika biashara kubwa kwa kusaidiwa na serikali bila ya kutoa rushwa.

Mfanyabiashara huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), alisema yeye aligoma kutoa rushwa kwa watendaji wa serikali jambo lililosababisha kupoteza fursa nyingi ambazo zingemfanya awe na maendeleo zaidi ya aliyonayo hivi sasa.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam wakati akichangia mada katika uzinduzi wa ripoti ya uchumi na maendeleo barani Afrika kwa mwaka 2013, uzinduzi uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Diplomasia.

Alisema kutokanana na kukithiri huko kwa rushwa, maendeleo ya kibiashara na kijamii hapa nchini hayawezi kufikiwa kama jitihada za kupambana na rushwa zitapuuzwa.

“Ili ufanikiwe ni lazima uione fursa iliyopo, lakini tatizo liko wapi mnajua… ni kwa hawa waliopewa dhamana ya kutoa vibali kuendekeza rushwa,” alisema Mengi.

Alisema ni vigumu katika nchi iliyojaa rushwa kuzungumzia suala la amani wakati wananchi wanapata huduma mbovu kutokana na watendaji wa serikali, taasisi na idara zake kuendekeza rushwa.

Alibainisha kuwa idara nyingi za serikali hivi sasa zimegubikwa kwa rushwa kiasi cha kuathiri huduma mbalimbali zitolewazo huku akitolea mfano wa matumizi ya bajeti ya serikali ya sh trilioni 18 yaliyoidhinishwa na Bunge hivi karibuni.

“Tunaweza kuangalia dhamira nzuri ya serikali hasa katika bajeti ya trilioni 18, manunuzi ya umma ni asilimia 80. Kati ya hizo asilimia 20 -30 zinaweza kuishia katika mianya ya wizi na rushwa, na mambo haya yanaweza kufanywa na watu wachache huku wengi wakiangamia kwa kukosa huduma muhimu,” alisema.

Alisema mbali na fedha zinazopotea katika manunuzi ya umma, maeneo mengine yanayofanya madudu kwa kiasi kikubwa ni sekta ya bandari, TANESCO na reli ambako alibainisha kuwa wajanja wachache wanatumia fursa walizonazo kujitengenezea mianya ya kufaidi rushwa ya maeneo hayo.

Aliongeza kuwa mianya ya rushwa isipodhibitiwa Mtanzania wa kipato cha chini ataendelea kuumia hata kama kipato chake kitaongezeka.

Alisisitiza kuwa tatizo jingine linalochangia rushwa nchini ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutokutambuliwa katika katiba pamoja na kunyimwa uwezo wa kuwashitaki watoaji na wapokeaji wakubwa wa rushwa.

Alisema katika kupambana na rushwa nguvu ya TAKUKURU inaishia katika kuwashitaki watuhumiwa wadogo, huku wakubwa wakisubiri uamuzi wa Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP).

Mengi alisema ana wasiwasi kuwa kwa hali ilivyo sasa kwenye sekta ya madini nchini hakuna Mtanzania atakayebaki miaka michache ijayo iwapo mambo hayatabadilishwa.

Alibainisha kuwa sera na kauli zinazotolewa midomoni mwa viongozi zinaelekeza kumuwezesha Mtanzania katika fursa mbalimbali wakati uhalisia wa matendo yao hauendani.

“Viongozi wanasema mdomoni kuwa wanataka kuwawezesha Watanzania, lakini ukweli ni kwamba kuna mkakati wa kuwarudisha nyuma kwa kasi kubwa,” alisema Mengi.

Awali, Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI), Felix Mosha akiwasilisha ripoti ya uchumi na maendeleo 2013 kwa bara la Afrika alisema ukosefu wa miundombinu bora katika bara hilo unachangia kwa kiasi kikubwa wawekezaji kushindwa kuwekeza katika maeneo yatakayoweza kumkwamua mwananchi wa kawaida.

Alisema nchi imefanya makosa makubwa kupuuzia kilimo cha kisasa na kukimbilia kuwekeza katika sekta nyingine huku ikiwaacha watu takribani asilimia 80 katika mbio za kuelekea katika mafanikio.

“Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 duniani na katika Afrika ni kati ya tano bora ambayo uchumi wake unakuwa kwa kasi kubwa, lakini wananchi wake wanaendelea kuwa katika hali duni. Hii ni kwa kuwa uwekezaji unafanywa katika maeneo yasiyowashirikisha wananchi moja kwa moja,” alisema Mosha.

TANZANIA DAIMA


Saturday, July 27, 2013

Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, Rais Jakaya Kikwete ametangaza operesheni kali ya kuwasaka majambazi wanaojihusisha na uhalifu ikiwemo utekaji wa magari na wahamiaji haramu itayoanza wiki mbili zijazo



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameamuru majambazi na wahamiaji haramu wote katika mikoa mitatu nchini kujisalimisha katika muda wa siku 14 kuanzia, Ijumaa, Julai 26, 2013 kabla ya kuanza kwa operesheni kubwa kuliko zote katika historia ya Tanzania nyenye lengo la kukomesha ujambazi katika mikoa hiyo na kukamata wahamiaji haramu.

Rais Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu amesema kuwa leo ametoa amri kwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama nchini kuanza maandalizii ya operesheni hiyo na hatimaye kuiendesha katika Mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita.

“Majambazi wanateka magari, wanaua watu wetu, wanapora mali zao. Watanzania hawawezi kuendelea kuishi kwa hofu, woga na taabu katika nchi yao wenyewe. Tutawasaka majambazi misituni, tutawasaka majumbani, tutachimbua ardhini kutafuta hata silaha zilizofukiwa chini,” amesema Rais Kikwete.

Rais Kikwete ametoa amri hiyo mchana wa jana, Ijumaa, Julai 26, 2013 wakati alipohutubia wananchi wa mjini Biharamulo, Mkoani Kagera, kabla ya kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa barabara ya lami kutoka Kagoma, Wilaya ya Muleba kwenda Lusahuga, Biharamulo.

Rais Kikwete ametoa amri hiyo kufuatia matukio ya mara kwa mara na yasiyokuwa na mwisho ya majambazi kuteka mabasi, kuua watu na kupora mali zadi katika mikoa hiyo, hali ambayo imesababisha malalamiko ya wakazi wa mikoa hiyo.

Rais Kikwete ameaambia wananchi: “Tumeamua kukomesha upuuzi huu katika mikoa ya Kagera, Kigoma Geita. Leo nimetoa maagizo kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama – Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi, Uhamiaji na Usalama wa Taifa kuandaa operesheni maalum, operesheni kubwa kuliko zote tokea tupate uhuru. Upuuzi huu hauwezi kuendelea.”


Friday, July 19, 2013

Rape in Dubai sets off outcry in Norway



News this week that a young Norwegian woman had been jailed in Dubai after reporting a rape there last spring has led to strong protests, also against the Norwegian government. Critics claim Norwegian officials should lodge a formal protest with the Dubai authorities for violating the woman’s human rights, while Norway’s foreign minister claims he already has “reacted strongly.”...


CHADEMA WATOA TAMKO KUHUSU MADAWA YA KULEVYA. TAMKO LA WAZIRI KIVULI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MHE. VINCENT JOSEPHAT NYERERE (MB) KUHUSU UDHAIFU WA SERIKALI KATIKA KUKOMESHA BIASHARA HARAMU YA MADAWA YA KULEVYA NCHINI.


Vincent Josephat Nyerere (Mbunge); Waziri kivuli mambo ya ndani (CHADEMA)


Ndugu wanahabari, kwanza kabisa napenda kuwashukuru kwa kuitikia wito wangu, ili niweze kuzungumza na watanzania kupitia kwenu kuhusu hatari kubwa inayolikumba taifa ya madawa ya kulevya.

Biashara haramu ya dawa za kulevya imekua kwa kasi sana hapa nchini miaka ya hivi karibuni licha ya kuwa na vyombo lukuki vya ulinzi na usalama na licha ya kuwa na Tume maalumu ya kudhibiti madawa ya kulevya chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda, iliyosomwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera Uratibu na Bunge Mhe. Wiliam Lukuvi tarehe 26 Juni, 2013 siku ya maadhimisho ya kitaifa ya kupiga vita dawa za kulevya huko Dodoma ni kwamba katika kipindi cha mwaka 2008 hadi 2012 watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya hapa nchini. Aidha, watanzania wapatao 240 walikamatwa na madawa ya kulevya katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika ya kusini na hivyo kutia doa taswira ya Tanzania katika jumuiya ya kimataifa. Kutokana na kukithiri kwa biashara hii haramu, Serikali kupitia maadhimisho hayo ya siku ya kupiga vita madawa ya kulevya duniani ilitangaza kuwa biashara ya dawa za kulevya kuwa ni janga la taifa. 

Mtakumbuka pia  kwamba hivi majuzi,  muda mfupi baada ya Serikali kutangaza kuwa biashara ya dawa za kulevya ni janga la taifa , walikamatwa wasichana wawili ambao ni watanzania huko Afrika ya kusini wakiwa na kilo 150 za madawa ya kulevya yenye thamani ya zaidi ya randi milioni 42.6 sawa na zaidi ya   shilingi bilioni 6 za kitanzania.

Ndugu wanahabari, matukio yote haya yametokea ndani ya kipindi cha miaka sita tu ya utawala wa Serikali ya awamu ya nne ambapo kuna viongozi wa juu Serikalini ambao waliwahi kusema kuwa wanawajua watu wanaojishughulisha na biashara haramu ya dawa za kulevya lakini mpaka sasa hawajawataja wahusika na wala hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi ya wahusika.

Ndugu wana habari, miongoni mwa viongozi wa  serikali na taasisi nyingine  waliosema kuwa wanawafahamu wafanya biashara ya madawa ya kulevya ni:-
Rais Jakaya Kikwete, ambaye alipiga hatua kubwa zaidi na kusema anawajua hata viongozi wa dini wanaofanya biashara hiyo. Licha ya maaskofu na viongozi wengine wa dini kumtaka Rais awataje wahusika hao wa madawa ya kulevya  ili kuuweka ukweli wazi, Rais hajafanya hivyo mpaka sasa.

Kamishna wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya: huyu alisema anayo majina ya vigogo (kwa maana ya viongozi) wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya lakini hajaweka majina hayo hadharani na wala haijulikani kama wahusika hao wamechukuliwa hatua yoyote hadi sasa.

Mbunge wa Mwibara – Kange Lugola alisema katika bunge la bajeti 2013/2014 kuwa kama Rais na Kamishna wa tume ya kudhibiti dawa za kulevya wanawajua “kwa majina” watu wanaojihusisha na biashara za dawa za kulevya na hawataki kuwataja watu hao wala kuwachulia hatu yamkini watu hao ni miongoni mwa mawaziri ndio maana kuna kigugumizi cha kuwataja na kuwachukulia hatua. Tangu Mhe. Kange Lugola alihusishe baraza la Mawaziri na kashfa hiyo ya kuhusika na biashara ya dawa za kulevya hakuna hatua yoyote ilivyochuliwa na Serikali kuthibitisha au kubatilisha kauli hiyo.

Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi  aliwahi kutoa taarifa ya wazi kuwa kuna kundi la matajiri wanaoshirikiana na viongozi wa Jeshi la Polisi waliokuwa wanapanga njama za kumwekea mtoto wake dawa za kulevya ili wambambikizie kesi ya dawa za kulevya na hivyo kuchafua heshima ya Bw. Mengi na familia yake. Ndugu mengi alisisitiza katika taarifa yake kwamba yuko tayari kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi na mamlaka nyingine zinazohusika ili kubaini njama hizo na kuchukua hatua stahiki kwa wahusika lakini mpaka leo Ndugu Mengi hakuhojiwa ili kuthibitisha kauli yake jambo linaloashiria kwamba kuna ukweli katika kauli yake.

Baada ya matukio yote haya na baada ya Serikali kukaa kimya kuhusu matukio hayo, mimi kama Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ya Nchi na kwa niaba ya Kambi  Rasmi ya Upinzani Bungeni ninatoa tamko kama ifuatavyo:

Rais Jakaya Mrisho Kikwete awataje na kuwachukulia hatua watu aliosema anawafahamu wanaojishughulisha na biashara ya dawa za kulevya la sivyo akubali kubeba shutuma kwamba Serikali yake ndio Mratibu Mkuu wa biashara ya dawa za kulevya ndio maana anashindwa kuchukua hatua.

Kamishana wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya awajibike kwa kutoa maelezo kwa umma juu  ya hatua alizochukua dhidi ya wahusika wa biashara ya dawa za kulevya aloiosema anawafahamu la sivyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni italazimika kuwashawishi wananchi kuamini kwamba  yamkini na yeye yumo katika mtandao wa wafanya biashara haramu ya dawa za kulevya ndio maana anasita kuwachukulia hatua wahusika hao ambao alishakiri kuwa anawafahamu. 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege awajibike kwa kutoa maelezo kwa umma kuwa ni tatizo gani linaloikabili mamlaka yake hadi kufanya viwanja vya ndege vya Tanzania kuwa ndio njia rahisi ya kuingiza na  kusafirishia madawa ya kulevya katika ukanda wa Afrika Mashariki?

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini na Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi wawajibike kwa kutoa maelezo kwa umma  kuwa ni kazi ipi wanayofanya ikiwa madawa ya kulevya yanaingizwa nchini  na kusafirishwa nje ya nchi kwa kasi kubwa zaidi?

HITIMISHO: Ni vema kama taifa tukatambua madhara ya madawa ya kulevya kwa vijana wetu ambao ndio nguvu kazi ya taifa. Kupuuzia na kutochukua hatua kwa wahusika wa dawa za kulevya ni kuangamiza nguvu kazi ya taifa. Nguvu kazi ya taifa ikishaharibiwa na dawa za kulevya hatuna taifa tena. Hivyo Serikali ifahamu kwamba kuendelea kulifumbia macho jambo hili kwa manufaa ya mafisadi wachache ni kulihujumu taifa na huo ni usaliti dhidi ya kiapo ilichokula cha kulitumikia taifa na kusimamia usitawi wa wananchi wa Tanzania. Aidha, Serikali itambue pia kwamba kuendelea kukaa kimya bila kuchukua hatua yoyote juu ya jambo hili kunatoa dalili kwamba yamkini ya yenyewe inahusika na biashara hiyo.

MUHIMU: IKIWA SERIKALI ITAENDELEA KUPUUZIA JAMBO HILI AMBALO LINALIANGAMIZA TAIFA, BASI KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI ITAENDESHA OPERESHENI NCHI NZIMA  ILI WANANCHI WAPIGE KURA KWA WAHUSIKA WAKUU WA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA, NA BAADA YA ZOEZI HILO, TUTAANIKA HADHARANI (KWA KUWATAJA MAJINA) WAHUSIKA WA BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA.

______________________________________
Vincent Josephat Nyerere (Mb)
MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI
NA WAZIRI KIVULI WA MABO YA NDANI YA NCHI
Imetolewa leo, tarehe 16 Julai, 2013


Thursday, July 18, 2013

Tanzania has maintained that it still owns half of Lake Malawi, reiterating that the border between the two countries runs in the middle of the disputed lake.



BLANTYRE (MaraPost) —Tanzania has maintained that it still owns half of Lake Malawi, reiterating that the border between the two countries runs in the middle of the disputed lake.

Tanzania’s foreign affairs and international cooperation, Mkumbwa Ally on Tuesday told that country’s Daily News Dodoma will not change its position on the matter.

“We didn’t expect anything new or different; neither are we going to change our position. Our position is that the border runs in the middle of Lake Nyasa/Malawi.

“The mediation team is gathering information, then they will give their statement, then each side will decide to take it further if they do not agree with the mediation team’s judgment,” Ally is quoted as saying.

The African Forum for Former Heads of State delegation are scheduled to leave for Tanzania next week on a fact-finding mission regarding the wrangle over sovereignty of Lake Malawi.

Former Mozambican President Joachim Chissano and Thabo Mbeki of South Africa on Sunday met President Joyce Banda and her entourage at Kamuzu Palace in Lilongwe on the same mission.

The Malawi leader told the two mediation team being led by Chissano to reach an agreement on the matter by this September or else the matter should go to the International Court of Justice (ICJ).

She said the longer the matter is taking to be resolved, the more strains are rising, mostly along the lake shores bordered with Tanzania.

President Banda also said her government will not bow down to “entertain any interim agreement” on usage of the waters of the lake with Tanzania “until the sovereignty issue is amicably resolved” through the SADC forum.

Banda notified Chissano and Mbeki that Malawi owns the entire lake except for a portion ceded to Mozambique in 1954 for mutually beneficial reasons.

Malawi, which sits to the west of Africa’s third-largest lake, claims the entire northern half of the lake while Tanzania, to the east, says it owns half of the northern area. The southern half is shared between Malawi and Mozambique.



Kurasa za mbele za baadhi ya magazeti ya Tanzania, Alhamisi 18 Julai 2013