Monday, December 30, 2013

Ernest Mangu, ameteuliwa kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi nchini, akichukua nafasi ya Said Mwema ambaye anastaafu wadhifa huo




Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyokabidhiwa Rais Jakaya Kikwete Jumatatu, 30 Desemba 2013


Waziri Mkuu Mizengo Pinda - Kiti moto!





Kilimanjaro Tourism Trade Fair Event - Oslo Norway 10-12 January 2014 


WE ARE HAPPY TO INVITE ALL FRIENDS OF TANZANIA TO THE ANNUAL 

NORWEGIAN TRAVEL AND TOURISM TRADE FAIR EXPO 2014. VISIT TANZANIA 

WILL EXHIBIT AT STAND NUMBER 550 WITH OTHER SAFARI AND FLIGHT 

COMPANIES REPRESENTING TANZANIA TRAVEL AND TOURISM INDUSTRY. WE 

WILL DISTRIBUTE FREE INFORMATION ABOUT TANZANIA TRAVEL, 

ADVENTURE, HOLIDAYS AND OTHER TOUR OF YOUR INTEREST TO THIS 

BEAUTIFUL COUNTRY. WE COVER TANZANIA MAINLAND AND ZANZIBAR. 


TICKERTS FOR ADULTS -50NOK AT ENTRANCE POINTS

CHILDREN UNDER 16 YEARS - FREE ENTRY

INVITE YOUR FRIENDS AND FAMILY AT STAND NUMBER 550



FOR FURTHER INFORMATION PLEASE CONTACT US AT 





Sunday, December 29, 2013

Shule yenye mwalimu mmoja tu chekechea hadi la saba yafaulisha wanafunzi wote darasa la saba



Katika hali isiyo ya kawaida, shule moja wilayani Bagamoyo imekutwa ikiwa na mwalimu mmoja tu anayefundisha wanafunzi kuanzia chekechea hadi darasa la saba, wote wakifundishwa katika chumba kimoja kwa kutumia ubao mmoja. Hata hivyo, katika matokeo ya Darasa la Saba Mwaka huu, wanafunzi wote 12 walifaulu kuingia kidato cha kwanza.

Shule hiyo ya msingi Machala, iliyokuwa na idadi ya wanafunzi 198 na imejengwa kwa majani kuanzia chini hadi kwenye paa.

Mwandishi wa habari hizi aliyetembelea shule hiyo, alimkuta mwalimu huyo akiwafundisha wanafunzi hao wa madarasa tofauti wakiwa kwenye chumba kimoja, huku ubao wa kufundishia ukiwa umechorwa mistari mitatu kutenganisha masomo ya chekechea hadi darasa la pili, mstari mwingine darasa la tatu hadi la tano na mwingine darasa la sita hadi la saba.

Mwalimu huyo, Christopher Rukutu, aliliambia NIPASHE Jumamosi kuwa shule hiyo hutumia kivuli cha mti kama ofisi.

Shule hiyo iliyopo katika kijiji cha Mihunga Kata ya Miono, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, ilianzishwa na serikali tangu mwaka 2007 ikiwa na wanafunzi 12 ambao wamemaliza darasa la saba, mwaka huu na kubahatika kufaulu wote.

Kwa mujibu wa mwalimu Rukutu, wanafunzi wote waliofaulu walipata alama za A na B isipokuwa mmoja aliyepata alama C. 

Pamoja na kuwa katika mazingira magumu, shule hiyo kiwilaya ilishika nafasi ya sita na kimkoa nafasi ya 20.

Alisema shule hiyo haina vitabu vya kiada wala vya kufundishia na amekuwa akiazima kutoka shule za jirani.

“Ninafundisha kwa akili za kuzaliwa sina kitabu cha mtaala wa elimu, nguvu zangu zote nilimalizia kwa darasa la saba ili wajue kusoma, kuandika na kuhesabu.

Kwa mwaka mzima sijafundisha darasa la nne nina wasiwasi matokeo yao hayatakuwa mazuri kwa sababu niko peke yangu," alisema kwa masikitiko.

Alifafanua kuwa tangu shule hiyo ianzishwe, serikali ilikuwa imewapanga walimu wawili tu, ambao kutokana na mazingira kuwa magumu waliripoti bila kuingia darasani na kuaga baada ya kuonyesha vyeti vya hospitali vinavyonyesha kuwa afya zao haziwezi kustahimili mazingira magumu.

Aliilalamikia serikali kuanzia ngazi ya kata hadi wilaya kwa kuisahau shule hiyo bila kuipa msaada wowote.

Mbali na kukosa msaada, shule hiyo pia inatumia tundu moja tu la choo kwa wanafunzi wa kike na kiume na kusababisha wengi wao kujisaidia vichakani.Alisema kutokana na hali hiyo, wanafunzi wengi hushambuliwa na ugonjwa wa kichocho.

Aliiomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kuwapangia wanafunzi wake 12 waliofaulu katika shule yake ya Machari kwenye shule za sekondari zenye mahitaji muhimu ili kuwapunguzia mateso wanafunzi hao.

Alisema wanafunzi wake hawajawahi kuona vitabu vya kujisomea na huduma muhimu za kiafya.


Chanzo: Nipashe, 28 Jumamosi 2013

Wednesday, December 25, 2013

Heri za Noeli




Tafakuri ya wazi juu ya Operesheni Tokomeza - Prof. Issa Shivji


Issa Shivji, Profesa Mstaafu wa Kigoda Cha Mwalimu Nyerere.


Aibu, aibu, aibu. … aibu ya kitaifa! Utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili uliosababisha mateso, ukatili, udhalilishwaji, upigaji na hatimaye vifo vya wananchi ni aibu kubwa kwa taifa letu. Sio aibu tu bali ni janga la kitaifa linalohitaji kufanyiwa tathmini na tafakuri na wananchi wote katika ujumla wao na kujiuliza: tunaelekea wapi?

Nini kimesababisha vyombo vya dola na mfumo wetu wa kisiasa kukosa kabisa uwajibikaji kiasi kwamba vyombo vilivyopewa jukumu la kuyalinda maisha, utu na heshima ya wananchi, vigeuke kuwa watesaji na wadhalilishaji wa wananchi hao hao! Kwa nini hatujifunzi? Kwa nini hatujirekebishi?

Katika historia yetu tumewahi kuwa na janga kama hili mnamo mwaka wa 1976 kutokana na Operesheni Mauaji huko Shinyanga na Mwanza. Mwalimu Nyerere aliwalazimisha viongozi wa kisiasa, akiwemo Mzee Mwinyi, kujiuzulu na watendaji wengine, wakiwemo wakuu wa jeshi la polisi na usalama katika ngazi ya mkoa, kuchukuliwa hatua za kisheria na kuadhibiwa ipasavyo. Tukio la operesheni Tokomeza linafanana sana na tukio la Operesheni Mauaji, lina sura ileile ya utesaji, udhalilishaji, ubakaji, na uporaji wa mali ya wananchi.

Matukio mengine ya aina hiyo, japokuwa hayakuwa makubwa kiasi hicho, yamewahi kutokea huko nyuma. Katika awamu ya pili,


1.    Kulikuwa na uaaji wa wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero mnamo mwaka 1986, na madhara na mateso waliyoyapata wananchi wakati wa Mwembechai. Katika awamu ya tatu ilitokea kashfa ya waandamaji huko Pemba kuuliwa na wengine kudhalilshwa kiasi kwamba tukio hili lilileta aibu kubwa sana kwa taifa. Kwa jumla, matukio kama haya, yaani utumiaji wa mabavu na vyombo vya mabavu – polisi, usalama, maaskari wengine kama wanamgambo, askari wa wanyama pori n.k. – yameongezeka awamu hadi awamu kiasi kwamba katika awamu ya nne tunashuhudia mauaji na mateso ya wanahabari na wananchi yakiongezeka mara dufu. Hili la operesheni Tokomeza ni kilele.

Sasa tufanyeje?


Uwajibikaji

Mawaziri wanne wamelazimishwa kuachia ngazi kwa kubeba dhamana ya kisiasa. Na wamepongezwa! Mengi mengine yanazungumziwa kwa mtazamo wa kichama na kisiasa. Wengine wanaenda mbali kusema kwamba Waziri Mkuu pia anatakiwa kujiuzulu. Haya yanaeleweka kwa sababu tukio lenyewe limeamsha hisia za watu na watu wanataka kuona waziwazi kwamba hatua za maana zinachukuliwa kuwatuliza.

Ni kweli kabisa kwamba tukio hili ni kashfa kubwa sana ya kitaifa. Katika mfumo wa kibunge (parliamentary system), Serikali nzima pamoja na mkuu wa serikali, yaani waziri mkuu, wangejiuzulu na labda uchaguzi mkuu ungeitishwa. Lakini katika mfumo wetu wa kirais (presidential system), mkuu wa serikali sio Waziri Mkuu. Ni


2.    Rais, na rais pia ni mkuu wa nchi. Kwa hivyo, kujiuzulu kwa Waziri Mkuu hakuna uzito. Kwa upande mwinigine, huwezi kutegemea rais mwenyewe na serikali yake kujiuzulu kwa sababu, rais pia ni mkuu wa nchi. Na huwezi ukawa nchi bila kiongozi mkuu; kutakuwa na ombwe la uongozi.

Kwa upande wangu, ili kuonyesha kwamba tukio hili linachukuliwa kwa uzito wake, na hisia za wananchi zinajibiwa zipasavyo, mambo mawili yafuatayo yanaweza kufanyika mara moja:

Moja, Rais kuvunja Baraza lake lote la Mawaziri, kama alivyofanya Mzee Mwinyi miaka ya tisini. Hatua hii itakaribiana na uvunjaji wa serikali. Hii itakuwa ni dalili ya uwajibikaji wa kisiasa.

Pili, watendaji, wakiwemo wale katika ngazi za juu, wafikishwe mbele ya mahakama kwa mashtaka ya kijinai. Mwanasheria Mkuu amependekeza uundaji wa Tume ya Kimahakama. Hii ni njia moja wapo lakini mara nyingi njia hii hutumika kama mbinu za kufunika kombe ili mwanaharamu apite. Nionavyo, labda safari hii, Rais Kikwete anaweza kutumia njia mbadala ya kuteua Mchunguzi huru (independent investigator and prosecutor) ambaye atakusanya ushahidi na kuandaa mashtaka ya kupeleka mbele ya Mahakama.

Na katika uchunguzi huu, watendaji wote wanaohusika, pamoja na wa kijeshi, usalama, na wa kiraia, wachunguzwe na kushtakiwa bila kujali nyadhifa zao.


3.    Tatu, jambo hili lizungumzwe na kujadiliwa na taifa zima kwa upana na undani wake bila kuficha au kulionea haya. Hakuna shule muhimu ya kujifunza kuliko shule ya umma. Shule ya Umma inafundisha na pia inasaidia kujenga maadili na uwajibikaji. Katika mijadala idara zitatajwa, watu waovu watasemwa kwa majina, maovu yanayofichwa uvunguni yatafichuliwa hadharani.

Mwishowe, ningependa kuligusia jambo moja muhimu ambalo linaonekana halijaguswa hata kidogo.

Dola na matumizi ya mabavu

Dola ni taasisi ya mabavu, popote pale duniani. Jeshi, polisi, maaskari wengine kama wa wanyama pori, wa hifadhi na kadhalika ni vyombo vya mabavu. Vyombo hivyo vya mabavu katika dola vinapata uhalali wa kisiasa kutumia mabavu kwa sababu vinadhibitiwa na kusimamiwa na vyombo na viongozi wa kisiasa ambao hupata uhalali wao kutokana na kuwa wawakilishi wa wananchi. Kwa mfano, jeshi la ulinzi hutumia mabavu kuilinda nchi dhidi ya maadui wa nje. Uwezo wa kutangaza vita na kuingiza jeshi vitani ni wa rais kama Amiri Jeshi mkuu; na rais ni kiongozi wa kisiasa aliyechaguliwa, sio mwanajeshi.

Katika mfumo wowote ule ambao ni wa kiraia, kwa maana kuwa sio wa kijeshi (military) au wa kipolisi (police state), vyombo vya kisiasa ndio hudhibiti na kusimamia vyombo vya mabavu. Jukumu la jeshi la ulinzi ni kuilinda nchi. Jukumu la jeshi la polisi ni kulinda amani,


4.    Wananchi na mali zao. Majukumu haya mawili ni tofauti na yanatenganishwa kikatiba. Hayaingiliani.

Ndio maana, jeshi la ulinzi halitumiki kudhibiti ghasia nchini. Hii ni kazi ya polisi. Katika mazingira ya kipekee ambayo kuna hatari ya serikali kupinduliwa kwa nguvu au kama kuna uasi ndio Jeshi la Ulinzi huingizwa mitaani. Na jambo hili hufanyika baada ya Rais kutangaza hali ya hatari kwa mujibu wa masharti ya katiba.

Kwa hivyo, ni kinyume na Katiba na mazoea mabaya kuliingiza jeshi la ulinzi katika mambo ya kiraia, kama vile uhalifu au ujangili. Kufanya hivyo ni kujenga mazoea mabaya na ya hatari sana.

Kinyume na msingi huu wa kikatiba, Operesheni Tokomeza ilichukuliwa kama operesheni ya kijeshi. Katika washiriki 2,371, wanajeshi walikuwa 885 au asilimia 37, yaani zaidi ya theluthi moja. Polisi walikuwa 480 au asilimia 20 tu. Wengine walikuwa kutoka majeshi mbalimbali kama la wanyapori n.k.

Pili, operesheni hii ilisimamiwa na Jeshi la Ulinzi. Na nikinukuu maneno ya Taarifa ya Kamati ya Bunge, “Taarifa za mwenendo wa operesheni zilikuwa zinapelekwa moja kwa moja kwa Mkuu wa Majeshi na kwamba, hazikumfikia Waziri wa Maliasili na Utalii.” Isitoshe, viongozi wa kisiasa kama wakuu wa wilaya na mikoa na viongozi wa kuchaguliwa kama madiwani, hawakushirikishwa wala hawakupewa taarifa zozote kuhusu operesheni hii. Mbaya zaidi, baadhi yao waliteswa na kudhalilishwa na maaskari waliohusika na


5.    Operesheni kiasi kwamba Mkuu wa Wilaya ya Ulanga alijificha katika hoteli.

Kwa kifupi basi, operesheni hii haikudhibitiwa wala kusimamiwa wala kuendeshwa kama operesheni ya kiraia (civilian operation), badala yake iliendeshwa kama operesheni ya kijeshi (military operation). Hili ni jambo la hatari sana na ni mazoea mabaya, hayakubaliki katika mfumo wa utawala wa kiraia (civilian government) .

Kuchanganya jeshi la ulinzi na mambo ya kiraia ni dhambi kubwa katika mfumo wa kisiasa tunaoufuata nchini mwetu. Jambo hili halikubaliki kabisa!.

Kwa hivyo, inashangaza kwamba hata Kamati ya Bunge haikuona hili na badala yake ikapendekeza kwamba Serikali iandaae “operesheni nyingine ambayo itapangwa na kutekelezwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Idara ya Usalama wa Taifa. ” Na hoja hii inaonekana kuungwa mkono bila kutiliwa shaka na wabunge wetu! Maana yake nini, wabunge hawajui na hawatambui kwa kuruhusu hili wanajenga mazoea hatari? Kama ndivyo basi ipo haja ya wanasiasa wetu pamoja na wabunge kujielimisha zaidi jinsi serikali za kiraia zilizochaguliwa na wananchi zinavyoendeshwa.


Angalizo! Tujihadhari, tusizoee kabisa kutumia Jeshi la Ulinzi katika mambo ya ndani kwa sababu kwa kufanya hivyo tutakuwa tunajenga mazoea hatarishi sana kwa mfumo wa kidemokrasia.



Monday, December 23, 2013

Sacking Kagasheki: The ultimate act of cover up in Tanzania


Mr. Khamis Kagasheki


By Prof. Dr. Wolfgang H. Thome, eTN Africa Correspondent | Dec 21, 2013

Tanzania's Minister for Natural Resources and Tourism, Amb. Khamis Kagasheki was sacked yesterday evening by Tanzania’s president Kikwete alongside three other cabinet colleagues, allegedly over the mishandling of anti poaching operations. Reactions were swift and united in calling this the ultimate act of a coverup, as Kagasheki was known as a minister full of integrity and backbone and had made a name for himself since replacing his hapless predecessor Ezekiel Maige.

‘Kagesheki wielded the axe in his ministry without fear or favour. He sacked those who were lazy and worked in cohoots with poachers and timber vandals. It is now clear to all of us that his remaining in office would have been a very big threat to those who organize poaching and profit from it and some are in the highest levels of government.
He was as usual the first to react
when reports filtered in that some of the operations in the field targeted herdsmen and pastoralists instead of poachers. He was right to then call for a temporary halt of such operations until new orders could be established.

He also stood up against very powerful interests over the Serengeti highway, the Lake Natron issue and other projects which endangered the principles of conservation in Tanzania. You wrote a lot about those issues and from what I read you always were very fair to our minister. He was an excellent minister and Kikwete surely must have succumbed to pressure to remove him because he was an obstacle to the evil schemes to keep poaching our wildlife and ransack our forests’ wrote a regular contributor from Dar es Salaam overnight, after the news broke that Kagesheki and his colleagues Mathayo (Lifestock and Fisheries), Nchimbi (Home Affairs) and Nahodha (Defence) had been sacked unceremoniously.

Another source wrote: ‘This makes Kagesheki the scapegoat. He is the one who reacted first when it became clear how the commanders in the field behaved. Some settled scores, others enriched themselves by stealing cattle. It was Kagesheki who stepped in and now he is being sacked? It shows that you were right that the entire operation Tokomeza was mishandled to make sure it had to be stopped. There are a lot of ulterior motives around and a lot of people who benefit from poaching are celebrating today that they brought him down. But for tourism and conservation it is a big blow. Some of the others may have been responsible but not Kagesheki’.

It is unprecedented that in one term of office a president in Tanzania sacks two of his ministers for natural resources and tourism in subsequent years, the first entirely justified of course but the second clearly done to please pressure groups with deep pockets bound to further benefit from this development.

Fare well and all the best to Ambassador Khamis Kagesheki, now immediate former Minister for Natural Resources and Tourism.



Sunday, December 22, 2013

Hotuba ya Zitto Kabwe - Kigoma: 21 Desemba 2013



Leo nina furaha kubwa sana kwani baada ya safari ndefu na yenye changamoto nimerudi nyumbani kuwasalimu wananchi wenzangu! Na hii si salamu za kawaida bali nawasalimu kwa salaam za demokrasia, uadilifu, uzalendo na uwajibikaji.

Nawasalimu si kama mbunge bali kama mwana wenu wa Kigoma! Na popote niendapo najivunia kujitambulisha kama Mtanzania; kama mwenyeji wa mkoa wa Kigoma na zao la Ujiji.

Tuna mengi ya kujivunia kama taifa lakini Ujiji na watu wake mna nafasi ya pekee katika historia. Watu wa Ujiji mlipokea harakati za kudai uhuru wa nchi yetu mapema kabisa mapambano ya uhuru yalipoanza. Watu wa Ujiji mlikuwa wa kwanza kabisa kupokea mfumo wa vyama vingi mwaka 1992. Na Jimbo la Kigoma Mjini ilikuwa miongoni mwa majimbo ya mwanzo kabisa kutoa mbunge wa CHADEMA mwaka 1995. Kabla ya hapo mlitoa madiwani wengi mwaka 1994.

Wakati Watanzania wengine wakiwa wanajiuliza mara mbili mbili kuhusu kujiunga na vyama vipya vilivyoanzishwa, watu wa Ujiji, watu wa Kigoma hamkusita kupokea mabadiliko. Wengi wamepoteza maisha yao, wengine kazi zao na wengine hata ndoa zao katika kupata mbegu ya mabadiliko katika nchi yetu. Nawataka msichoke. Wekeni nguvu mpya katika kusimika mabadiliko kwani bado kazi ya kuimarisha demokrasia katika nchi yetu haijaisha na inahitaji uvumilivu, kusameheana na kuaminiana.

Na nchi yetu Tanzania ni nchi inayoonyesha uwezo mkubwa katika kupendana, kuaminiana, kuvumiliana na hata kusameheana. Na haya si maneno tu ambayo ninayazungumza kama mwanasiasa. Hii ni hali halisi na maisha niliyoyaishi kwa mifano nilipokuwa ninakua na kusoma katika shule ya Msingi Kigoma na baadaye Shule ya Sekondari Kigoma.

Malezi yangu yalikuwa yanaongozwa na jamii nzima ya Kigoma. Nimekuwa nikiwaeleza rafiki zangu niliokutana nao kwenye masomo na kwenye siasa kwamba nimeanza kuvaa viatu kwa mara ya kwanza nikiwa darasa la tatu. Viatu hivyo viliitwa 'asante Salim' vilivyokuwa vinatengenezwa na Kampuni ya Bora Shoes. Vililinunuliwa na mama Coretha Furugunya ambaye tulikuwa tunakaa mtaa mmoja wa Kisangani Mwanga. Mama Coretha hakuninunulia viatu kwa sababu alikuwa ana uwezo mkubwa, la hasha! Alifurahishwa na matokeo yangu ya mitihani ya darasa la pili kwenda la tatu. Ninaamini kitendo cha mama huyu ni ushahidi wa uungwana, upendo na hata uwajibikaji ambao tunao sisi watanzania.

Uwajibikaji kwani alichukua jukumu kunilea ingawa hakuwa mzazi wangu, lakini aliona kuwa kama mwanajamii ana nafasi kubwa katika kuwaendeleza watoto wote. Jamii hii ya watu wa Kigoma ilinifunza kuwa nikijitahidi na kukazana kwa bidii kwenye masomo na majukumu, nitafanikiwa. Siwezi kusahau somo hili katika maisha yangu na ni somo hili ndilo limenifanya nijitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu kuwatumikia kwa uadilifu na mafanikio ya hali ya juu sana.

Nikiwa nimejaa matumaini haya kuhusu wananchi wenzangu, leo nataka niwakumbushe kwa nini kama jamii tulichagua kufuata njia ya demokrasia. Demokrasia ina maana pale ambapo inatumika kuleta mabadiliko chanya kwenye maisha ya wananchi. Maisha yanayotakiwa ni yale yanayomwezesha mwananchi kupata huduma zake stahili kama Elimu, Afya, Maji na miundombinu. Demokrasia haina maana pale wananchi wanakufa njaa kwa kukosa ajira na kukuza umasikini. Demokrasia inahusu maendeleo.

Tumejitahidi kwa upande wetu kuondoa mkoa wa Kigoma kutoka mikoa isiyo na miundombinu kabisa ya maendeleo mpaka kuwa mkoa unaotumika kama mfano kwa miradi mingi ya Maendeleo ikiwemo Daraja la Malagarasi, Uwanja wa ndege wa Gombe-Mahale, barabara za lami na upanuzi wa Bandari, ujenzi wa bandari ndogo mpya na ujenzi wa kituo cha Usafirishaji Mwandiga.

Asije mtu akasema yeye ndio kafanya haya. Haya ni matunda ya nyinyi watu wa Kigoma kupokea demokrasia na bila woga kuchagua viongozi wenu bila kujali vyama bali kwa kuangalia uwezo. Haya ni matunda ya viongozi wenu kupaza sauti yenu kwenye baraza la Taifa, Bunge. Haya ni matunda ya uvumilivu wenu na uamuzi wenu wa kutaka maendeleo. Juhudi hizi lazima ziendelezwe kwa nguvu zote ili kuhakikisha kuwa nafasi ya mkoa wa Kigoma katika uchumi wa Tanzania inaonekana dhahiri na hivyo kuchochea maendeleo ya nchi yetu kwa kuwa kituo cha biashara katika nchi za maziwa makuu.

Lakini tukumbuke pia kuwa Demokrasia ni Uwajibikaji. Katika kipindi cha utumishi wangu kwenu,kutokana na malezi niliyoyapata kutoka kwenu,nimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa Serikali inawajibika kwa Wananchi. Nakumbuka wakati napambana kuhusu sheria mbovu ya madini kuna watu hapa nyumbani walisema 'sasa huyu kawa mbunge wa Taifa' lakini watu wengi zaidi wakasema tumemtuma Dodoma kusemea Watanzania wote na sio Kigoma tu.

Tuliweza ndani ya miaka mitano kufanya mabadiliko makubwa sana kwenye sera ya Madini na sheria ya madini ambapo baadhi ya mambo ambayo yalikuwa hayafikiriki sasa yametungiwa sheria ikiwemo Serikali kuwa na hisa kwenye migodi, Tanzanite kumilikiwa na Watanzania sio chini ya asilimia 50 na kuzuia kabisa wageni kuchimba vito vya thamani.

Uwajibikaji ulipelekea kumshinikiza Rais kufanya mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri kwa kuwafukuza mawaziri wanane mwaka jana. Hii ilitokana sio tu na hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu bali pia ushiriki mkubwa wa wananchi kupitia simu na mitandao ya kijamii ambapo wabunge walishinikizwa kuweka saini kwenye karatasi za kumtoa Waziri Mkuu. Toka wakati huo kumekuwa na utaratibu sasa ambapo wabunge hawaoni taabu kutaka uwajibikaji waziwazi ili kuzuia ubadhirifu wa fedha za Umma. Ni hivi jana tumeshuhudia mawaziri wanne wamejiuzulu na kufukuzwa kazi kutokana na kashfa ya operesheni Tokomeza ujangili iliyoibuliwa na ripoti ya kamati ya bunge. Mabadiliko haya ni hatua muhimu katika kuimarisha demokrasia yetu.

Pamoja na matunda haya mengi mazuri lakini bado kuna changamoto katika juhudi zetu.

Changamoto kubwa tuliyonayo wananchi ni kukosekana kwa imani katika demokrasia yetu.

Kutoaminiana
Ni dhahiri kuwa kutoaminiana katika nchi yetu kumekuwa kwa kiasi kikubwa. Taarifa za kitafiti zinaonyesha kuwa katika kila Watanzania kumi, wanane hawaaminiani. Ni changamoto kubwa sana. Wananchi wameacha kutuamini wanasiasa na wanasiasa wameacha kuaminiana wenyewe kwa wenyewe. Hivi sasa uongo umegeuzwa kuwa ukweli na ukweli umekuwa ni uongo. Hivi sasa ukitaka kuwa mwanasiasa maarufu inabidi ujue kudanganya na ukitaka kuitwa mwanasiasa msaliti inabidi uwe msema kweli.

Kukosekana kwa uaminifu na kuaminiana imekuwa ni kansa katika siasa zetu. Itachukua muda mrefu sana kujenga demokrasia imara katika nchi yetu kama hatutapata jibu la changamoto hii ya kutoaminiana na kugeuza uongo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo. Hivi sasa ukweli umekuwa unatengenezwa badala ya kutafutwa. Ni majanga! Juzi bungeni Mwanasheria Mkuu wa Serikali alielekeza shutuma kwangu kwamba sikushirikiana na kamati maalum iliyoundwa na Bunge kufuatilia mabilioni ya uswisi na kwamba chini ya kiapo nilisema sina majina ya watu wenye akaunti huko Uswisi. Huu ulikuwa ni uongo.

Ni uongo kwa sababu niliitika wito wa kamati hata nilipokuwa katika mafunzo ya mgambo huko Tanga na nilikutana nao mara nne. Ni uongo kwa sababu niliwapa wajumbe wa Kamati Maalaum maelezo na taarifa nyingi sana kuhusu utoroshwaji wa fedha nje ya nchi na umiliki wa mali nje ya nchi kinyumecha sheria.

Ni uongo kwa sababu mimi kutotaja majina haya haina maana sina majina, bali ni kwamba ninaheshimu utaratibu na nimeachia vyombo husika vikamilishe uchunguzi. Kwani mimi kama mtu binafsi nikianza kuchukua majukumu ya taasisi ninaweza kutia dosari harakati hizi muhimu na hata kupelekea mchakato mzima kuvurugika. Sitaingia mtego huu! Lakini hatua hii ya Mwanasheria Mkuu imenipelekea kujiuliza maswali mengi kwa mfano uongo kama huu ulifanywa kwa malengo gani? Na ninajikuta hata mimi ninaingia katika hali ninayoilalamikia ya KUTOAMINIANA.

Lakini mtambue pia kuwa kutoaminiana kunaleta kutovumiliana. Hivi sasa kuwa na mawazo tofauti katika vyama vya siasa au hata asasi za kijamii ni uhaini. Lakini bila kuenzi tofauti za mawazo hatuwezi kujenga vyama imara wala Taifa imara. Demokrasia imara ni zao la tofauti za mawazo na uhuru wa mawazo. Kama hatuwezi kujenga vyama vinavyorutubisha uhuru wa mawazo na tofauti za mawazo, tutajenga Taifa lenye watu wenye kuogopa na waliojaa woga. Wanachama wanapoogopa uongozi ni udikteta, lakini uongozi unapoogopa wanachama ni demokrasia. Bila demokrasia ya uwazi na kuvumiliana tutakuwa Taifa la kidikteta. Lazima vyama vya siasa, viongozwe kwa namna ile ile ambayo Taifa litaongozwa.

Demokrasia bila kuaminiana, demokrasia bila kuvumiliana sio demokrasia ya kweli. Juzi nilipoingia Bungeni kwa mara ya kwanza baada ya matukio kadhaa yanayoendelea ndani ya chama chetu nilikaa pamoja na mbunge Tundu Lissu. Wabunge wengine walidhani tutarushiana ngumi na badala yake ikawa ni vicheko na mazungumzo. Hii ni kwa sababu sina chuki na mtu yeyote yule.

Mmenifunza kutojenga chuki na watu na badala yake kuchukua kila tukio kama changamoto ya maisha. Siasa ni kupambanisha mawazo tofauti na hatimaye kutafuta suluhu ya pamoja. Na siasa ina misingi yake ambayo sisi wanasiasa huwa tunasahau kwa maksudi. Msingi wa siasa ni kuwa inapaswa kuleta unafuu wa maisha ya wananchi na sio malumbano tu ya kurushiana maneno na kuzushiana ili kujijengea umaarufu wa kisiasa. Siasa si kuwekeana chuki na kuonyeshana ubabe.

Na hapo ni muhimu muelewa wanaKigoma mnapoambiwa kuwa eti ninapofuatilia mabilioni ya Uswisi ninatafuta umaarufu, ni uongo! Mnaposikia eti kukataa kwangu kuchukua posho ni unafiki na kujitafutia umaarufu, ni uongo! Kinachonisukuma kufanya vyote hivi ni ninyi. Ninasukuwa kila ninapowaona watoto bado wanatembea bila viatu; kila ninapoona akina mama wanapoteza maisha yao katika uzazi;kila ninapoona vijana ambao hawana uhakika wa kupata hata mlo moja kwa siku kwa kukosa kazi; ninapoona wazee wa Kigoma kukosa hata shilingi mia moja kununua chai asubuhi. Ninawaona si wanaKigoma bali mamilioni ya watanzania wakiishi katika hali hii. Alafu nalinganisha na taarifa tunazozipata kuhusu ufujaji na utoroshwaji wa pesa zetu.

Hebu sasa linganisheni na ukweli kuwa ripoti ya kimataifa iliyotolewa hivi karibuni imeonyesha kuwa mwaka 2010 pekee, jumla ya dola za kimarekani milioni 1315 (bilioni 1.3), yaani shilingi trilioni 2,113,930,000,000 (sh trilioni 2.1) zilitoroshwa kutoka nchini Tanzania.

Mwaka 2011 kiasi cha dola za kimarekani milioni 817 yani shilingi za kitanzania zipatazo trilioni 1,315,370,000,000 (trilioni 1.3) zilitoroshwa. Ripoti hiyo inaeleza kuwa jumla ya fedha za Watanzania zilizotoroshwa nje ya nchi katika miaka kumi iliyopita zilifikia dola za kimarekani milioni 4526 (bilioni 4.5) sawa na shilingi za kitanzania trilioni 7,286,860,000,000 (trilioni 7.3).

Nimewatajia hapa namba chungu nzima na matrilioni na mabilioni hayaleti maana. Lakini hii ina maana kwamba kiasi cha pesa zilizotoroshwa katika miaka 10 pesa - robo yake tuingeweza kujenga barabara ya lami ya kiwango cha juu kabisa kutoka Kigoma mpaka Dar-es-salaam!

Pesa hizi zingeweza kuajiri na kuwalipa vizuri walimu, madaktari na wafanyakazi wengine ili kuhakikisha tunapata huduma bora na kutengeneza ajira bora kwa vijana wetu. Pesa hizi zingeweza kununua madawa muhimu na kuokoa maisha ya maelfu ya akina mama tunaowapoteza kila mwaka wakati wa uzazi. Pesa hizi zingeweza kuwanunulia watanzania wote si watoto tu angalau pea 10 ya viatu. Sasa nikitafakari haya siwezi kuchapa usingizi mnono na kufumbia macho utoroshwaji wa fedha au matumizi mabaya ya fedha za umma kwa njia ya sisi wabunge kujilipia posho! Hapana! Nafsi yangu hainiruhusu kukaa kimya kwa kuogopa kuitwa mbinafsi au msaliti!

Lakini naomba niwasihi kuwa katika nyakati kama hizi za changamoto za kisiasa jambo la msingi kuliko yote ni kutulia maana hakuna linalotokea bila sababu. Licha ya kwamba kuna watu wengi wanapaza sauti zao katika mambo haya lakini pia kuna wengi zaidi ambao wapo kimya lakini wana mawazo yao, ndani na nje ya chama chetu;ndani na nje ya Serikali na ndani nanje ya nchi yetu. Ndio maana lazima kuibadili nchi yetu ili kuweza kuhakikisha kila raia anakuwa na fursa ya kutoa mawazo na fikra zake zinakuwa huru.

Maisha ni mabadiliko; mabadiliko hayana ukomo; mabadiliko hayazuiliki kwa sababu bila mabadiliko hakuna ukuaji, bila mabadiliko hakuna maendeleo. Mabadiliko ni kiu kikubwa cha Tanzania kwa sababu mabadiliko huleta matumaini. Na kiu hii ni kubwa zaidi kwetu sisi vijana wa kizazi hiki kipya. Siasa za kizazi kipya cha viongozi ni siasa za majawabu ya kero za wananchi. Siasa za mabadiliko ni siasa za kujenga na kuimarisha; ni siasa za kuaminiana na kuheshimiana hata pale mnapopingana kimawazo. Ninataka tujenge siasa mpya Tanzania;siasa za mabadiliko; siasa zinazojenga matumaini ya kweli;siasa zinazowajali na kuwajengea uwezo wananchi wa Tanzania.

Mungu ibariki Tanzania.


Saturday, December 21, 2013

Waziri Mkuu ndg. Mizengo Pinda asema kuwa Rais Jakaya Kikwete amekubali kutengua nyadhifa za mawaziri wanne baada ya ripoti ya "Operesheni Tokomeza"



Waziri Mkuu wa Tanzania, Ndugu Mizengo Pinda amesema kuwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekubali kutengua nyadhifa za mawaziri wanne baada ya ripoti ya "Operesheni Tokomeza". Ripoti hiyo ilitolewa Bungeni mjini Dodoma. 

Mawaziri waliotenguliwa nyadhifa zao ni: 
1. Davida Mathayo David; waziri wa Mifugo na Uvuvi,
2. Khamis Kagasheki; waziri wa Maliasili na Utalii,
3. Emmanuel Nchimbi; waziri wa Mambo ya Ndani na
4. Shamsi Vuai Nahodha; waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Thursday, December 19, 2013

Kutoka Jamii Forums - kama ni kweli...tunakoelekea ni kubaya!!!


Theo Mutahaba - kuhusu ufuska wa MM, Viongozi wa CCM na Wabunge wanawake wa CCM.


Zitto Kabwe.

Nataka ujue kwamba kati ya watu 10 wajinga au wapumbavu, utakuwa mmoja wao. Nakushangaa kila siku unajigamba una akili. Akili gani uliyonayo
wakati unanunuliwa na watu wapumbavu kama Mwigulu Nchemba. Unashirikiana na TISS pamoja na makada wakubwa wa CCM, utajuaje kama mimi siyo moja ya hao watu? Au kwa sababu unajuana na Jack Nzoka? Jack ndio nani? Mwigulu pamoja na ushamba wake, amekutega vibaya na ukanasa kama swala. Ona jinsi anavyokutumia na kundi lako la Masalia kwenye mitandao ya kijamii

Zitto umekuja hadharani na propaganda za kijinga na kudai kwamba nimekutishia maisha, nilikutishia wapi wakati nilikuonya tu kwamba uwe mwangalifu na CCM pamoja na TISS unaoshikiana nao? Wakishakuua, watakuja kudai kwamba CHADEMA ndio waliokuua? Hivi wewe ni mzima kweli kijana? Mwisho ukaja kudai mimi mmoja wa vifaranga? Kijana kuwa mwanagalifu umefika pabaya kisiasa. Afadhali utafute njia mbadala. Muulize Mwigulu alifuata nini Uchini na Yule balozi anawasaidia CCM kwenye kazi gani?

Mimi kama mmoja wa watu wanaokujua vizuri na usaliti wako, zaidi yako unavyojijua, nakwambia wazi kabisa kwamba vijana wenye uwezo wa kuliongoza hii nchi tulishawaona. Haumo kabisa kwenye kundi hilo. Hiyo tuliliona siku ulipopokea magari ya Rostam Aziz. Mwenye uwezo mkubwa zaidi kuliongoza Tanzania anaishi nje ya nchi, haeleweki ataingia siasa au hataingia, na wala haeleweki kwamba yumo kwenye chama gani. Mwingine ambaye yuko karibu na anaomeonyesha uwezo, yuko CHADEMA. Wengine wote ni kelele tu kama wewe, Kilaza Nchimbi na Mlevi na Fisadi January Makamba

Bwana Zito, ukitaka kujua ujinga wako, ni pale ulipomparamia mke wa Kagasheki ambaye ameshindana na Nape Nauye. Umeingia kwenye mtego wa Mwigulu Nchemba pamoja na ushamba wake. Unajua kwamba Catherine Magige ni mke wa Kagasheki. Baada ya Conference yako kuhusu kutimuliwa Chadema, uliondoka na Catherine Magige na Binti yake mdogo mkaenda Dubai siku kadhaa kabla hajaenda uingereza ambako ametoka siku tatu nne zilizopita. Dubai ulifuatwa hadi kwenye hoteli mlikofikia.

Camera zilisetiwa na kurekodiwa mkifanya ngono na sehemu nyingine nyingi. Siyo wewe tu, Nape Nauye pia amerokodiwa akifanya Ngono na Catherine. Ngeleja amerekodiwa akifanya Ngono na Anna Kilango Malechela. Zitto nilishiriki binafsi kukurekodi ukifanya ngono na Eliza Luhanjo Marekani, sasa kazi kwako kijana…Muendelezo wa mitego dhidi ya kuwanasa na kuwazima wapumbavu kama wewe…..Tuone. Umerekodiwa na mara nyingi sana na watu tofauti pale Sinza unakolala na kila rangi ya mwanamke ……Hivi zile plani zako za kijinga Kigoma sasa hivi, unajua kweli baadhi ya wale vijana wanaoratibu ni wana TISS? Simu zote za kijinga unazompigia kakako na misukule mingine yote inarekodiwa, kwa jinsi ulivyompumbavu

Ili kukukomesha baada ya kunitaja hadharani, ninakuhakikishia kwamba ninayo video mkononi. Sasa tuone nani mjanja. Hii kitu ni muda tu tutampa Kagasheki ajionee na baadae viongozi wote wa CCM.hatutakurupuka. tutachukua muda wetu, hasa kabla ya uchaguzi wa 2015, Kwa sababu maneno tu utasema sisi waongo . Ulidhani kwamba wewe mjanja, lakini kumbe ni mtu mwepesi sana. Usichezee watu usiowaona. Mtandao huu ni mkubwa, tuko kila sehemu unakokwenda.Hakuna anayekuopenda TISS wala CCM. Unatumiwa tu. Stakabadhi ya fedha ulizotumiwa ujerumani tunazo…………..Umechokoza watu wenye uwezo zaidi ya TISS. Baada ya malalamiko kupelekwa Ujerumani, sasa hivi EU nzima inaku monitor na huyo ghaidi mshamba Mwigulu ambaye umeshirikiana naye kwembe mambo mengi ya hujuma na ughaidi

Ili CHADEMA ibaki kuwa chama, lazima wakufukuze. Yaani ni lazima wakuvue uanachama kwa maana hata wewe pia hilo unalijua, wamegundua baadhi ya mambo yako lakini siyo yote. Mpango wa TISS kukutumia kuwaua viongozi wake unalijua? CHADEMA watakuwa wajinga sana kama hawata kufukuza na wana mabadiliko hawatawaelewa. Hujuma unazowafanyia zimetosha. Ulishiriki kutaka kumuua Mbowe Arusha, CHADEMA Hawalijui hilo. Zitto wakina Kileo, ni wewe ndiye uliyesuka mpango mzima wa kuwasweka Lwakatare na Kileo. Tunasubiri wakufukuze, alafu na sisi pia tuingilie kati ka kuwaambia wana CCM kwamba hauwafai, mtafuta sifa za kijinga. Na kwa taarifa yako maongezi yako ya hivi karibuni na Andrea tangu sakata la CHADEMA lianze tunayo !

Hii email itapokewa na zaidi ya watu 50.nimefanya makusudi, na kama utabisha haukwenda Dubai na Catherine Magige, niko tayari kuweka scanned copies za ticket zenu na hoteli mliyofikia