Wednesday, June 18, 2014

Mohammed Ali (KTN Kenya) amwandikia barua Rais Uhuru Kenyatta, jana Jumanne 17.06.2014Kenya imegeuka sasa na kuwa shamba la wanyama.shamba ambalo wanyama wote ni sawa lakini wengine ni bora zaidi. Kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa Kenya imekuwa ikikumbwa na msukosuko wa ugaidi, uhalifu, mauaji ya kiholela na ufisadi. Wanaojipata kubanwa ni wakenya walala hoi. Kuanzia Tana River, Baragoi, Westgate hadi Mpeketoni. Ni nani mtetezi wa wakenya? Hii leo mwanahabari wetu mpekuzi Mohammed Ali amwemwandikia barua Rais Uhuru Kenyatta na kumtaka akaze njuga na awakomboe Wakenya wanaouawa kinyama kila kukicha.


No comments: