Wednesday, July 02, 2014

Waziri wa uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe awatimua kazi wafanyakazi 13 wa uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere - East Africa Television (EATV)Waziri wa uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe (pichani) atangaza kuwafukuza kazi watumishi 13 wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa makosa ya ukiukwaji wa taratibu za kazi, rushwa pamoja na kuchukua mali haramu na kusaidia kupitisha bidhaa mbalimbali kwa njia za magendo. Mwakyembe amesema vita dhidi ya upitishwaji wa madawa ya kulevya umeanza kufanikiwa.


Mwakyembe aliwataja wafanyakazi hao kuwa ni: Teddy Mwasenga, Esther Kilonzo, Rehema Mrutu, Mary Kadokayosi, Kisamio Sami, Aneth Kenonga, Agnes Shirima, Hamis Bora, Valeria Chuwa, Elengira Mghase, Remedius Kakulu,  Eshy Ndossi na Ane Setebe.

Chanzo: East Africa Television (EATV) saa 11 jioni leo Jumatano, 02.07.2014


No comments: