Saturday, October 25, 2014

From Summertime to Wintertime in Norway: Time conversion date Sunday 26th.October 2014 CET (Central European Time). Adjust the time from 03:00 CET back to 02:00 CET - Tunaingia saa za majira ya theluji (Wintertime) kuamkia Jumapili, 26.Oktoba 2014




Saa 9 usiku kuamkia Jumapili, 26.Oktoba 2014, hapa Norway (Skandinavia) tunabadili majira na kuingia majira ya theluji (Wintertime). Kufuatia na mabadiliko ya majira, tunarudisha saa moja nyuma. 

Tuna tofauti ya masaa mawili na saa za Afrika Mashariki (East African Time = EAT) kwenye majira ya theluji. 

Mfano:

Hapa Norway ikiwa saa 4 za asubuhi,

Tanzania (Afrika Mashariki) ni saa 6 za mchana... 

Mabadiliko ya saa hufanyika mara mbili kwa mwaka.



Jumapili ya mwisho ya Machi, kuingia majira ya Kiangazi (Summertime). Tunasogeza saa moja mbele. Tofauti ya saa moja na Afrika Mashariki.


Jumapili ya mwisho ya Oktoba, kuingia majira ya theluji (Wintertime). Tunarudisha saa moja nyuma. Tofauti ya masaa mawili na Afrika Mashariki.


1 comment: