Wednesday, December 31, 2014

Balozi wa Tanzania nchi za Nordic na za Baltic Bi.Dora Msechu atatoa hati za utambulisho kwa Mfalme Harald V wa Norway Alhamisi 15.01.2015. Balozi Msechu anaomba kukutana na Watanzania na wenye asili ya Utanzania waishio Norway Jumamosi 17.01.2015.


Balozi Dora Mmari Msechu ni Balozi wa Tanzania kwenye za Nordic (DenmarkFinlandIcelandNorway na Sweden) na sehemu zinazojitawala, the Åland Islands, the Faroe Islands and Greenland) na nchi za Baltic (Estonia, Latvia na Lithuania).


Balozi wa Tanzania nchi za Nordic na za Baltic Bi.Dora Msechu atatoa hati za utambulisho kwa Mfalme Harald V wa Norway Alhamisi 15.01.2015. Balozi Msechu anaomba kukutana na Watanzania waishio Norway Jumamosi 17.01.2015. 

Mahali na saa, watu watajulishwa siku zikikaribia.


Watanzania waishio Norway wenye pasipoti za Tanzania zinazoisha muda wakati wowote ule mwaka 2015 wanaombwa kuja mapema sehemu tutakayokutana na Balozi Msechu Jumamosi 17.01.2015 ili ubalozi uwashughulikie kuhusu maombi 
ya pasipoti mpya.

A. KUHUSU PASIPOTI MPYA:

1. Watakaokuwa kwenye mchakato wa kubadilisha pasipoti walipe kabla kabla ya siku hiyo SEK.600,- kwa kupitia kwenye akaunti ya ubalozi http://www.tanemb.se Na hiyo siku waje na risiti ya malipo ya hizo Kroner za Kiswidi (SEK)

2. Waliopoteza pasipoti walipe SEK.1100,- kwenye akaunti ya ubalozi (http://www.tanemb.se) . Kwa waliopoteza pasipoti zao, waje na uthibitisho wa kiserikali kuonyesha kuwa walioa taarifa pasipoti zilipopotea.

3. Kwa waombaji waje siku hiyo na MOSI: Pasipoti inayokwisha muda wake. PILI: Kopi ya ukurasa wenye picha na kopi ya kurasa namba 1 hadi 5.

4. Waombaji waje na kopi ya kibali cha kuishi.

5. Waombaji waje na picha 5 saizi ya pasipoti za rangi ya bluuu au bluu bahari.

B. KWA WATAKAOOMBEA WATOTO WAO WAJE NA:

1. Kopi za pasipoti za wazazi wote wawili (kama ni mzazi pweke kopi ya pasipoti mzazi pweke inatosha) hata kama mzazi/wazazi wana pasipoti za Kinorwejiani au za nchi ingine. Kuna wazazi wenye watoto walio na pasipoti za Tanzania hii inawahusu endapo watapenda watoto wao kuendelea kuwa na pasipoti za Tanzania.

2. Kopi iliyothibibitishwa na Notarius Publicus ya cheti cha kuzaliwa. Kopi iwe kopihalisi na iwe imetafsiriwa kwa Kiingereza.

3. Picha 5 saizi ya pasipoti za rangi ya bluu au bluu bahari.

No comments: